Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waziri Mkuu Pakistan jela miaka saba

Muktasari:

Kesi iliyokuwa ikimkabili Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan, Nawaz Sharif, imetolewa hukumu leo Jumatatu ambapo waziri huyo amekutwa na hatia ikiwamo ya kumiliki nyumba jijini London.

Islamabad, Pakistan Mahakama inayoshughulikia kesi za rushwa nchini Pakistan, imemhukumu kwenda jela miaka saba Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan, Nawaz Sharif, baada ya kumkuta na hatia kwenye mashtaka ya rushwa yaliyokuwa yakimkabili.

Mahakama imemkuta na hatia leo Jumatatu Waziri Mkuu huyo, ambaye ameongoza nchi hiyo kwa awamu tatu tofauti, baada ya kushindwa kuthibitisha vyanzo vyake vya mapato, ikiwamo umiliki wa kiwanda cha chuma huko Saudi Arabia, shirika la habari la Geo limeripoti.

Awali, Sharif alihukumiwa kwenda jela miaka 10 mwezi Julai na mahakama hiyo hiyo, kutokana na mashtaka yaliyofanana na haya ya sasa ambayo ni kununua nyumba maeneo ya matajiri jijini London, Uingereza baada ya mahakama ya juu kumuondoa madarakani.

Waziri Mkuu huyo wa zamani alitolewa gerezani mwezi Septemba baada ya kukata rufaa katika kesi iliyokuwa ikimkabili.


Mwandishi wa Aljazeera aliyepo Islamabad, anaripoti kuwa upande wa mlalamikiwa ambaye amehukumiwa, unaona kwamba hukumu hiyo imetokana na uhasama wa kisiasa na kwamba uamuzi huo wanauchukulia kwa uzito.

“Mahakama imetangaza kuwa atahukumiwa kwenda jela miaka saba katika kesi ya umiliki wa kiwanda cha chuma cha Al-Azizia, wakati amekutwa hana hatia kwenye kesi nyingine,” alisema.

“Hili ni suala linalopaswa kutazamwa kwa umakini sana na chama chake. Hata hivyo, ikumbukwe kwamba Nawaz Sharif alikamatwa akishtakiwa kumiliki mali huko Avenfield, akapelekwa gerezani na baadaye kuachiwa kwa dhamana,” aliongeza.