Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Benki ya Dunia yaipa Tanzania Sh1.2 trilioni mkopo nafuu

WB yaipa Tanzania Sh1.2 trilioni mkopo nafuu

Muktasari:

  • Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Benki ya Dunia (IDA) leo Mei 27, limesema mkopo huo utaiwezesha Tanzania kufanikisha maeneo hayo chini ya Mradi wa Ushirikiano wa Usafiri Tanzania (TanTIP) utakaowezesha pia taasisi husika katika kupanga na kusimamia sekta hiyo.  

Dar es Salaam.  Serikali imeendelea kuonyesha matumaini ya kuimarisha huduma za kijamii nchini baada ya kupata mkopo wa masharti nafuu wa Sh1.2trilioni utakaofungua milango ya kuboresha usalama, ustahimilivu wa tabianchi, uwezo wa barabara za ndani na viwanja vya ndege vya Mikoa.

Taarifa iliyotolewa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Benki ya Dunia (IDA) leo Mei 27, imesema mkopo huo utaiwezesha Tanzania kufanikisha maeneo hayo chini ya Mradi wa Ushirikiano wa Usafiri Tanzania (TanTIP) utakaowezesha pia taasisi husika katika kupanga na kusimamia sekta hiyo.  

Imesema ufadhili huo utasaidia uboreshaji na ukarabati wa barabara zenye urefu wa kilomita 500, zikiwemo za Mtwara-Mingoyo-Masasi (kilomita 201), Lusahunga-Rusumo (kilomita 92), Songea-Rutukila (kilomita 111) na Iringa-Msembe (kilomita 104), huku ikishughulikia hali ya hewa ili kuongeza ustahimilivu wa barabara.

Pia fedha hizo zitatumika katika uboreshaji na ukarabati wa viwanja vitatu vya ndege vya kipaumbele vya mikoa: viwanja vya ndege vya Lake Manyara, Iringa na Tanga kwa kuzingatia usalama na uwezo wake.

Taarifa hiyo pia imetaja  uendelezaji wa uwezo wa kitaasisi ikijumuisha usimamizi na usalama wa hali ya hewa, kuhimiza usawa wa kijinsia, ushirikishwaji wa fursa za maendeleo ya kazi kwa wanawake na kusaidia utekelezaji wa mradi, usimamizi na ufuatiliaji.

Akizungumzia msaada huo, Mkurugenzi mkazi wa Benki ya Dunia Mara Warwick amesema hatua hiyo itachochea mafanikio ya Tanzania katika muongo mmoja uliopita yaliyotokana na faida muhimu za eneo lake la kimkakati la bahari, maliasili, utulivu wake wa kijamii na kisiasa, na ukuaji wa haraka wa sekta ya utalii," alisema

“Uwekezaji chini ya mradi huu utachangia juhudi kubwa zaidi za serikali katika kuboresha muunganisho wa uchumi wa Tanzania na uhusiano wake na majirani zake na soko la kimataifa, sambamba na kuhakikisha miundombinu inabadilika.”

Naye Gylfi Palsson ambaye ni mtaalamu Mkuu wa Usafiri wa Benki ya Dunia alinukuliwa katika taarifa hiyo akisema: "Mradi utaimarisha hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuzingatia masuala ya kustahimili hali ya hewa katika mipango, uwekezaji na usimamizi wa sekta ya usafiri wa barabarani.”

Mradi huu utafaidi moja kwa moja jumuiya na makampuni mengi, ikiwa ni pamoja na wakulima wadogo, waendeshaji biashara ya kilimo, wawekezaji waliopo na wanaoweza kuwa wawekezaji wa sekta binafsi, waagizaji na wauzaji bidhaa nje.

“Pia itakuwa na matokeo chanya katika maendeleo ya ustawi wa kiuchumi, ushirikishwaji wa kijamii, usawa na ubora wa mazingira,” amesema.