Wizara yaagiza kunawa mikono, matumizi ya vipukusi

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Waziri wa Afya, Dk Dorothy Gwajima amewataka Watanzania kuimarisha usafi wa mtu mmoja mmoja na mazingiran kwa kunawa mikono kwamaji tiririka na sabuni, kujifukiza na kutumia vipukusi ‘sanitizer’.

Dar es Salaam. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Dorothy Gwajima amewataka Watanzania kuimarisha usafi wa mtu mmoja mmoja na mazingiran kwa kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni, kujifukiza na kutumia vipukusi ‘sanitizer’.
Dk Gwajima amesema hayo leo Jumatatu Februari Mosi, 2021 jijini Dodoma wakati akitoa tamko lake kufuatia taarifa za uwepo wa mlipuko wa pili wa ugonjwa wa corona, Covid19 katika nchi jirani ambapo amekuwa akipokea maswali mengi kutoka kwa wanahabari
Amesema Wizara inawakumbusha kujielekeza kwenye elimu ambayo imekuwa ikitolewa na wataalamu wa afya ambayo pia itaendelea kutolewa.
“Lazima kuimarisha usafi wa mazingira, mtu mmoja mmoja, kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni, kutumia vipukusi, kujifukiza, kufanya mazoezi mbalimbali, kula lishe bora, kula matunda ya kutosha, maji kwa wingi na tiba asili ambazo taifa letu limejaaliwa kwa maana tunazo tiba asili mbalimbali,” amesema Dk Gwajima na kuongeza;
“Kupitia Mkemia Mkuu wa Serikali Wizara imefanya kazi ya kukagua bidhaa kadhaa za tiba asili ambazo zimeshakidhi viwango vya usalama kwa ajili ya matumizi, tayari zinatumika na wengi zimewasaidia ikiwemo mimi na familia yangu.”
Pia, Dk Gwajima amezitaka taasisi binafsi, za kidini na vyama vya siasa kuepuka kutoa taarifa za afya ambazo hazifuati miongozo ya wizara, “Tunayo miongozo wakishatoa taarifa hizo zinaleta taharuki, taasisi hizi zote tunazitaka kuacha kutoa taarifa zozote au kuchukua maamuzi.”