Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yas yatua Mlima Kilimanjaro

Moshi. Kampuni ya Yas Tanzania imeimarisha nafasi yake kama mwekezaji kinara katika sekta ya mawasiliano nchini kupitia kampeni maalum ya upandaji Mlima Kilimanjaro. Kampeni hiyo, iliyohusisha wafanyakazi 16 wa kampuni hiyo, ni sehemu ya juhudi za kutangaza nembo mpya ya kampuni hiyo na kuonyesha dhamira yake ya kuendelea kuwekeza Tanzania. 

Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini wa Yas Tanzania, Henry Kinabo, amesema mazingira mazuri ya uwekezaji nchini yameiwezesha kampuni hiyo kufanikisha juhudi zake za kuboresha huduma na kuvutia wateja.

“Tanzania ina mazingira bora ya uwekezaji, na Yas Tanzania inajivunia kuwa sehemu ya maendeleo haya. Kupanda Mlima Kilimanjaro ni ishara ya dhamira yetu ya ubora na utambulisho wetu wa Kiafrika,” amesema Kinabo. 

Kampeni hiyo ililenga kuimarisha utambulisho wa chapa ya Yas, iliyozinduliwa upya Novemba 26 mwaka huu, baada ya mabadiliko ya nembo kutoka Tigo. Washiriki wote wa safari hiyo, wakiwemo wanawake watatu, walifanikiwa kufika kilele cha Uhuru, ambapo walipandisha bendera za Yas na "Mixx by Yas" kama alama ya mafanikio. 

Kinabo alisisitiza kuwa hatua hiyo pia inalenga kusaidia juhudi za serikali katika kukuza sekta ya utalii kwa kutangaza Mlima Kilimanjaro kama kivutio kikuu cha utalii duniani.

“Kupanda mlima huu ni ujumbe wa nguvu kuhusu dhamira yetu siyo tu ya kuboresha huduma za mawasiliano, bali pia kusaidia kukuza sekta nyingine muhimu kama utalii,” ameongeza. 

Akizungumzia mafanikio ya kampeni hiyo, Kiongozi wa safari hiyo, Emmanuel Mallya, amesema imeonyesha uimara wa wafanyakazi wa Yas Tanzania na azma yao ya kuendelea kuboresha huduma kwa wateja.

“Tumekusudia kuboresha mtandao wetu kwa uwekezaji wa takriban Sh1 trilioni tukilenga kuhakikisha huduma za mawasiliano zinawafikia Watanzania wa vijijini na mijini kwa kiwango bora,” amesema Mallya. 

Washiriki wa safari hiyo walieleza kuwa uzoefu huo ulikuwa wa kipekee na wenye changamoto.  Evelyn Gamasa, mmoja wa washiriki, aliwataka Watanzania kuthamini utalii wa ndani kwa kutembelea vivutio kama Mlima Kilimanjaro. 

Kwa upande wake, Ofisa Rasilimali Watu wa Yas, Florah Kivuyo, alisema mafanikio ya timu hiyo yanadhihirisha ubora wa Yas kama chapa ya Kiafrika inayolenga kutoa huduma bora kwa wateja wake.

“Safari ya timu yetu kufika kilele cha Afrika ni alama ya dhamira yetu ya kufanikisha malengo ya kampuni na kuimarisha huduma za mawasiliano nchini,” amesema.