Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zahanati Manispaa ya Morogoro zapatiwa vifaa tiba

Mbunge wa Morogoro Mjini AbdulAziz Abood, akikabidhi kifaa tiba (Microscope), kwa diwani wa Kata ya Mbuyuni Manispaa ya Morogoro, Samuel Msuya. Picha Lilian Lucas.

Muktasari:

  • Vifaa vya maabara vimetolewa kwenye zahanati saba kati ya 30 zilizopo Manispaa ya Morogoro vitakavyosaidia wananchi kuacha kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya vipimo

Morogoro. Wakati Mbunge wa Morogoro Mjini Abdulaziz Abood akitoa vifaa tiba kwa ajili ya maabara wilayani hapa, changamoto iliyopo ni kukosekana kwa wataalamu katika baadhi ya zahanati zilizopokea vifaa hivyo.

Changamoto hiyo imejitokeza Oktoba 31, 2023 kwenye ziara ya mbunge huyo ambapo ametoa vifaa tiba vyenye thamani ya Sh9.3 milioni kwa zahanati za Kingolwira, Sultan, Mbuyuni, Kichangani, Sabasaba, Tungi na Lukobe.      

Abood amuomba Mganga Mkuu wa Manispaa ya Morogoro, Maneno Focus kuhakikisha zahanati na vituo vya afya vinapata wataalamu wa maabara na kuondoa changamoto iliyopo.

“Naamini wataalamu wakipatikana tutatatua changamoto hii na kama inashindikana nitaongea na mkurugenzi tushirikiane kuiomba Wizara ya Afya ituletee haraka,” amesema.

Kwa upande wake Focus amesema Serikali imeendelea kuboresha huduma za afya kwenye maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa wataalamu wa kada zote za afya na vifaa tiba.

Amesema pamoja na kwamba awali kulikuwa na changamoto ya uwapo wa vituo lakini vikajengwa, changamoto ikawa vifaa tiba lakini vinaendelea kuletwa.

Dk Focus amesema baadhi ya watumishi wanaendelea kuwapokea na Serikali imeendeea kuahidi kuleta wengine.

“Kupitia mfuko wa jimbo, umeweza kupeleka fedha na kununua vifaatiba, hiyo ni hatua kubwa na inaongeza utoaji huduma kwenye maeneo mengi ndani ya manispaa na kupunguza malalamiko ya wananchi,”amesema Dk Focus.

Ametaja vifaa vilivyotolewa na mbunge Abood kuwa ni kifaa cha kuangalia vimelea vya wadudu, kifaa cha kuchakata sampuli zinazochukuliwa kutoka kwa mgonjwa na kifaa cha kupima sukari.

Dk Focus amesema kati ya zahanati na vituo 30 vya Serikali vinavyotoa huduma vituo 12 ndio vilikuwa vikitoa huduma ya maabara na sasa vituo 19 zitakuwa vinatoa huduma hiyo baada ya mbunge kutoa msaada kwenye maeneo hayo.

Diwani wa Mbuyuni Samuel Msuya amesema changamoto iliyokuwapo awali, ni kupata huduma ya vifaa vya maabara na kulazimika kwenda maeneo mengine, hivyo wananchi watakuwa na uhakika wa huduma na kuwapunguzia mwendo.

“Wapo wagonjwa wengi walikuwa wanafika, lakini kutokana na kukosekana na vipimo walikuwa wanalazimika kuondoka, pamoja na kutupatia vifaa hivi bado tutakuwa na changamoto ya mtaalamu wa maabara,"amesema Msuya.