Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zaidi ya wanafunzi 200,000 wahitimu mafunzo ya ualimu

Naibu Waziri katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi

Muktasari:

  • Serikali imesema katika kipindi cha 2016 hadi Desemba 2020 jumla ya wanafunzi 248,379 walihitimu ngazi mbalimbali za masomo ya ualimu.

Dodoma. Serikali imesema katika kipindi cha 2016 hadi Desemba 2020 jumla ya wanafunzi 248,379 walihitimu ngazi mbalimbali za masomo ya ualimu.

Naibu Waziri katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi ameyasema hayo leo Jumatano Aprili 20, 2022 wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Same Magharibi (CCM), Dk David Mathayo.

Katika swali alihoji; “ni lini Serikali itatoa vibali vya kuajiri walimu wa kutosha kukabiliana na ongezeko la wanafunzi na wahitimu? Wangapi wapo kwenye soko la ajira”

Akijibu swali hilo, Ndejembi amesema walimu hao walihitimu katika ngazi za astashahada, stashahada na shahada na kati, wameajiriwa na Serikali na wengine sekta Binafsi.

Amesema 2021/2022 Serikali imetoa kibali cha nafasi 10,003 za ajira kwa walimu.

Aidha, 2022/2023 Serikali imepanga kutoa kibali cha ajira kwa nafasi 30,000 zikiwemo nafasi za waalimu.