Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Namna ya kuepuka uteja wa kujichua

Dk Shita Samwel

Muktasari:

Tatizo hili kwa lugha ya kiingereza linaitwa ‘musterbation’. Linaonekana zaidi kwa vijana kuanzia miaka 16-18 na kuendelea lakini ukweli hata watu wazima wapo wenye tabia ya kujichua.

Kujichua ni tatizo la kitabia ambalo ninaulizwa mara kwa mara na wasomaji hasa vijana.

Tatizo hili kwa lugha ya kiingereza linaitwa ‘musterbation’. Linaonekana zaidi kwa vijana kuanzia miaka 16-18 na kuendelea lakini ukweli hata watu wazima wapo wenye tabia ya kujichua.

Ni kweli jambo hilo linampatia mtu hisia nzuri lakini nikinyume na utaratibu wa kawaida wa mwanadamu. Ikifikia hatua ya mtu kuwa mteja wa kujichua, hawezi kuishi hivyo kusababisha muingiliano wa maisha ya mtu katika utu na imani.

Mpaka hapo hilo linakuwa ni tatizo kubwa na linahitaji urekebishaji wa tabia hiyo.

Hatua za kufuata kumtoa mtu kwenye tabia hiyo

Njia ya kwanza ni kwa muathirika anatakiwa keupuka kujilaani na kujiona yeye mkosaji pekee katika tatizo hili. Utafiti unaonyesha karibu asilimia 95 ya wanaume wamewahi kufanya kitendo hiki maishani mwao. Jichukulie wewe ni binadamu kama wengine, kukosea na kujisahihisha na kurudi katika mstari mnyoofu ni jambo la kawaida maishani.

Hata pale unapojaribu kujirekebisha mara kwa mara ukashindwa, unapaswa kujipongeza na siyo kujikatia tamaa, kujikataa na kujiona mkosaji.

Njia ya pili, kaa mbali na vitu au mambo yanayokufanya kushawishika kufanya tendo hilo ikiwamo picha au video za ngono, mitandao ya picha za utupu na makundi ya marafiki wenye kupendelea kufanya jambo hilo. Kama unajikuta unakifanya kitendo hicho wakati wakuoga, wakati wa usiku au asubuhi sana, hakikisha unabadili ratiba hiyo.

Kama ni mazingira ya usiku mwingi ukiwa peke yako na huna shughuli yakufanya, jaribu kujiepusha kwa kujitengenezea kazi zitakazo fifisha mawazo ya kufanya tendo hilo. Njia ya tatu, jichanganye na jamii kwa kuweka ratiba maalumu ili usiwe mpweke ama kukosa raha.

Upweke unaongeza ushawishi wa kufanya tendo hilo hasa kwa wale ambao wanafanya kama mbadala baada ya kukwaruzana katika mahusiano au kuachana na wenza wao. Tengeneza ratiba yakwenda mahali kama vile kusali, kutazama mpira, kufanya mazoezi, kujisomea vitabu na kusalimia ndugu, jamaa na marafiki. Njia ya nne, jipangie ratiba ya kujishughulisha na mambo mengine yenye tija na huku ukitengeneza hulka mpya zitakazofifisha mawazo yakukumbuka kufanya tendo hilo.

Mfano hulka hizo ni pamoja na kujiunga na klabu za mazoezi au kujifunza vifaa vya muziki, kuogelea, klabu za vijana za kazi za kujitole na michezo ya kujilinda kama karate. Jikite katika malengo ya baadaye yatakayokufanya uwe na maisha ya furaha. Weka juhudi kuyafikia malengo hayo na fanya kazi au soma kwa bidii ili ufaulu. Njia ya tano; kumbuka utakapoanza kujishughulisha na kazi mbalimbali ili kukabiliana na tatizo hilo utahitaji mlo kamili unaofuata kanuni za afya ili uwe na afya njema.

Jaribu pia kuongeza kula vyakula unavyokula mara chache, yaani matunda na mboga za majani, hii itakufanya ujisikie mwenye kujitambua na kujiona umehamia maisha mapya.

Mlo kamili unaipa pia nguvu akili yako inayotumia nishati nyingi unapokuwa na msongo wa mawazo ili kukabiliana na tatizo la kujichua. Njia ya sita; kuwa mvumilivu kwani ni vigumu kuacha kujichua kwa ghafla. Jipe muda kuhakikisha unajibidiisha katika kutatua tatizo hili.

Kama itatokea umejaribu na ukashindwa, hupaswi kujilaumu bali piga moyo konde na uamini utashinda. Njia ya saba; tafuta ushauri nasaha kutoka kwa watu unaoweza kuwaamini ikiwamo ndugu waliokuzidi umri, wazee wenye hekima na busara, viongozi wa dini na walimu wako hasa wa malezi.

Kama njia hizi zikishindwa kukusaidia fika hospitalini uonane na daktari kwa msaada zaidi wa kiafya.