Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fahamu sababu ya kutoka na damu kwenye fizi

Muktasari:

Mara nyingi ufizi wenye tatizo hili huwa na rangi nyekundu tofauti na rangi ya kawaida ya pinki ya ufizi wenye afya.

Ugonjwa wa fizi kutoa damu ni ile hali ya mtu anapopiga mswaki ama kung’ata kitu, huacha alama ya damu kwenye kitu kilichong’atwa.

Hali hiyo hutokana na ufizi husika kuvimba.

Mara nyingi ufizi wenye tatizo hili huwa na rangi nyekundu tofauti na rangi ya kawaida ya pinki ya ufizi wenye afya.

Kwa kuwa ugonjwa huu hasa katika hali ya mwanzo unaweza usionekane kuwa tatizo kwako, lakini inakupasa utambue kuwa ufizi wenye afya njema hautoi damu wakati wa kupiga mswaki ama uking’ata kitu.

Hivyo, ni muhimu kuchukua hatua mapema ili kuitibu hali hiyo mara unapoibaini.

Hii ni kwa sababu ugonjwa huu unapoendelea, huweza kuathiri mfupa wa taya sehemu ambayo jino hujishika na kusababisha kulegea au kung’oka.

Wataalamu wa afya ya kinywa na meno wanasema ufizi wenye afya una rangi ya pinki iliyopauka. Kama fizi zimevimba na zinakuwa na rangi nyekundu na kutoa damu kirahisi, inawezekana kabisa mhusika akawa na tatizo la ugonjwa wa fizi.

Kwa kua ugonjwa huu mara nyingi hauna maumivu, mtu anaweza akadumu nao kwa muda mrefu bila kujua.

Dalili ya maradhi haya

Ni fizi kuwa na rangi nyekundu hasa katika maeneo zinapokutana na jino, kuacha alama ya damu mtu anapong’ata kitu kigumu kama embe bichi, kutoa damu wakati wa kupiga mswaki. Wakati mwingine anaweza kuona damu kwenye mswaki.

Inashauriwa umuone daktari wa kinywa na meno mara kwa mara, ili kutambua maradhi ya kinywa na meno kama unayo.

Maradhi hayo ni pamoja na kuvimba fizi na kutoa damu na meno kutoboka.

Lakini kabla hayajaleta madhara zaidi, unatakiwa kuwahi hospitali kuonana na wataalamu kwa tiba na ushauri.

Katika muktadha wa kuvimba fizi, unapohisi kuwa una dalili za ugonjwa huo, muone daktari mapema.

Inaelezwa kuwa sababu kubwa za ugonjwa huo ni ile hali ya kinywa kutokuwa safi, hivyo husababisha utando laini kujijenga kwenye meno na kuendelea kujiimarisha. Utando huo katika hali ya awali, unaweza usiuone.

Hii ni kwa sababu unakuwa umejengwa na bakteria wanaopatikana kinywani. Utando huo mlaini hutengenezwa wakati bakteria walioko kinywani wanapokutana na vyakula vinavyoliwa kila siku.

Kwa kuwa ni mlaini, mtu anashauriwa kupiga mswaki mara mbili kwa siku pamoja na kuflosi ili kuuondoa kwa urahisi.

Tabaka hili laini linahitajika kuondolewa kila siku kwa sababu hujijenga haraka ndani ya saa 24.

Tabaka hili laini linapokaa kwa muda mrefu kinywani, huanza kukomaa na kutengeneza ugaga kwenye meno ambalo ni tabaka gumu. ,Ugaga husababisha ugumu kwa tabaka laini kuondoka na hata kusaidia kujenga hifadhi kwa bakteria.

Huwezi kuondoa ugaga kwa kupiga mswaki ama kuflosi. Wataalamu wa kinywa na meno wanasema ni lazima kwenda kwa daktari kwa msaada zaidi.

Kwa kadiri tabaka laini na ugaga linavyojishika kwenye meno, ndivyo ufizi unavyozidi kuumia na kuvimba na hatimaye kutoa damu na huweza kusababisha pia kutoboka kwa meno.

Hata hivyo ni lazima kutambua kuwa ugonjwa huu ni wa kawaida na mtu yeyote anaweza kuugua. Wengi huupata kwa mara ya kwanza kipindi cha balehe na kisha katika viwango tofauti maishani mwao.

Inaelezwa sababu zinazoweza kuongeza uwezekano wa kupata ugonjwa huo ni pamoja na kutokuwa na tabia ya kufanya usafi wa kinywa, ugonjwa wa kisukari, uzee, kupungua kwa kinga ya mwili kutokana na maambukizi ya virusi vya Ukimwi na mengineyo.

Inaelezwa kuwa maradhi hayo yanaweza kutambulika kwa kuchunguza kinywa cha mgonjwa husika.

Daktari huchunguza fizi, meno na ulimi pamoja na dalili za ugonjwa husika.

Pia ataangalia kama kwenye meno kuna tabaka laini ama ugaga, halikadhalika ataangalia rangi ya ufizi na hali yake ya kutoka damu kiurahisi ukiguswa na kitu ili kujiridhisha.

Kama kinywani kutakua hakuonekani tatizo, daktari atapendekeza kufanyika kwa uchunguzi wa kitabibu ili kujua chanzo hasa cha tatizo.

Ili kumaliza tatizo hilo, matibabu ya haraka hutakiwa kufanyika, ili kuondoa kabisa ugonjwa huo pamoja na dalili zake na kuzuia kuendelea.

Matibabu hayo yanapaswa kufanywa na daktari, huku mgonjwa akitakiwa kuhakikisha anafanya usafi wa kinywa vizuri akiwa nyumbani.