Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Namna ya kumsaidia mgumba kupata mtoto

Muktasari:

Nikitumia uwezo wangu wa kifedha nilifanikiwa kufika mpaka nje ya nchi lakini nikagundulika kuwa sina uwezo tena wa kuzalisha hali iliyonifanya niwe mnyonge.

Mimi ni mwanaume wa miaka 62 ni mmoja wa waathirika wa tatizo la ugumba, kwa muda mrefu nimekuwa nikihangaikia bila mafanikio kutatua tatizo hili.

Nikitumia uwezo wangu wa kifedha nilifanikiwa kufika mpaka nje ya nchi lakini nikagundulika kuwa sina uwezo tena wa kuzalisha hali iliyonifanya niwe mnyonge.

Nikashauriwa kutumia njia ya kupandikiza kwa mke wangu au kuamua kuasili mtoto. Lakini sina ufahamu wa kutosha wa njia hizi za kupandikiza kama ni salama na mke wangu atapata mtoto asiye na matatizo.

Ndugu wa msomaji huyo ni mmoja wa wafuatiliaji wa safu hii ya kona ya afya ya wanaume ambaye amekuwa akifuatilia makala za karibuni zinazohusu ugumba kwa wanaume.

Leo nitawapa ufahamu wa njia ya upandikizaji wa mbegu kwa njia ya kimaabara na hapo baadaye tutaona kama ni salama kwa mwanadamu.

Kama nilivyowahi kueleza hapo awali kuwa ugumba unaweza ukamwathiri mwenza yoyote ingawa jamii imezoea kumtupia lawama mwanamke wakati kumbe mwanaume pia anaweza kupata tatizo la ugumba.

Kwa wale wanaume ambao imeshindikana kabisa kupona na amekosa kabisa watoto kwa njia ya asili ya kawaida zipo njia ambazo zinazoweza kutumika na kuwapa watoto wakaishi maisha ya furaha.

Tukianzia na njia maarufu ya upandikizaji ijulikanayo kama In vitro fertilization (IVF) ni moja ya njia maarufu ya kitaalamu ambayo imekuwa ikitumika duniani kote kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa mimba kwa mgumba wa kike au wakiume. Njia hii pia hujulikana kama mtoto wa chupa (Test tube baby) ni njia ambayo hufanyika nje ya mwili wa binadamu katika maabara maalum kwa kuchukua yai la kike lililokomaa na kulipandikiza mbegu iliyokomaa.

IVF ni mojawapo ya njia saidizi za kutatua upatikanaji wa watoto ambazo hutumika kwa wenza wenye tatizo la ugumba ambao hawana watoto au wanahitaji kuongeza watoto baada ya njia ya asili kushindikana.

Yai la kike lililotungishwa huweza kurutubishwa na kukuzwa katika mazingira maalum kwa muda wa siku mbili hadi sita na kisha hapo baadaye huingizwa katika mji wa mimba wa mwanamke na kupachikwa katika eneo ambalo yai hujipachika kwa ajili ya kuanza kukua.

Njia hii hutumika endapo mwanaume ana tatizo la kuwa na mbegu zisizo na ubora au zisizo komaa hivyo kushindwa kutungisha yai la kike.

Njia hii pia inatumika kwa wanawake wenye vikwazo katika mirija yao ambavyo inasababisha kutungishwa kwa njia ya asili kuwa vigumu.

Mara zingine mayai ya kike au mbegu ya kiume zinaweza kuwa zimetoka kwa watu ambao hawana tatizo la ugumba ambao wanaojitolea kwa watu wenye matatizo ya ugumba.

Ingawa inaweza ikatokea mbegu ya kiume ya muathirika inashindwa kupenya katika kuta za yai tu, hapa mbegu hiyo inaweza kusaidiwa na vifaa maalumu na kupandikiwa katika maabara hiyo.

Njia kama hii humpa faraja muhusika kwani mbegu yake iliyobeba taarifa zake za kiurithi inarithiwa kwa mimba itakayotungwa. Ikumbukwe ya kwamba mtoto anayezaliwa huwa ni muunganiko wa nusu kwa nusu wa chembe za kiurithi kwa baba na mama.

Inawezekana tatizo ni mwenza mmoja tu ambaye ni mwanaume hivyo yai la kike likapandikizwa na mbegu ya mtu wa kujitolea yaani mwanaume mwingine kufuatana taratibu za kitabibu na miiko yake.