Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hii ndiyo aina ya mwanamume anayempenda Lady Jaydee

Mwanamuziki Judith Wambura maarufu Lady Jaydee

Muktasari:

Vyombo mbalimbali vya habari ikiwamo mitandao ya kijamii imekuwa ikiandika kuhusu kuyumba kwa uhusiano wa wawili hao, huku wengine wakienda mbali zaidi kwa kusema kuwa chanzo ni mume wa msanii huyo.

Kwa muda mrefu kumekuwapo na minong’ono juu ya mwanamuziki Judith Wambura maarufu Lady Jaydee kuachana na mume wake Gardner Habash ambaye ni mtangazaji wa redio E-Fm jambo ambalo halijawekwa wazi mpaka sasa na wawili hao.

Vyombo mbalimbali vya habari ikiwamo mitandao ya kijamii imekuwa ikiandika kuhusu kuyumba kwa uhusiano wa wawili hao, huku wengine wakienda mbali zaidi kwa kusema kuwa chanzo ni mume wa msanii huyo.

Ndani ya miaka 14 ya muziki, Februari 2015 ni mwezi ambao Lady Jaydee ameweza kufanya tukio la kihistoria baada ya kuwasiliana na mashabiki zake walio wengi kupitia mitandao ya kijamii.

Jaydee ambaye alihitaji kuwasiliana na mashabiki wake moja kwa moja kwa njia ya maswali, hakujali umbali, aina ya maswali wala nini mashabiki wake walihitaji kufahamu kutoka kwake.

Akitumia ukurasa wake wa Instagram, Jaydee alifanikiwa kuwajibu mashabiki wake maswali 10 waliyomuuliza kwa ufasaha, jambo ambalo hakuwahi kulifanya kabla.

Mwanamuziki huyo aliamua kufunguka na kuweka wazi kuwa kwa sasa anaishi na mtoto wa mdogo wake Dabo Laban na kwamba nyumbani kwake wako wawili tu lakini pia ameweka wazi kuhusu aina ya mwanamume anayempenda

Ingawa hakuenda kwa undani kuhusu mumewe kwa maneno hayo ni wazi kuwa kwa sasa hayuko pamoja na mumewe. Starehe kwa kuzingatia matakwa ya wasomaji wake imeoamua kuchapisha maswali hayo pamoja na majibu yake na hii ni sehemu ya mahojiano hayo;

Swali: Una mtoto au watoto na utazaa lini, tunasikia umeasili mtoto? Pia tunasikia una mtoto mkubwa uliyemzaa na kumuacha kijijini Shinyanga?

Jibu: Sina mtoto na sijajua mpaka sasa nitazaa lini, ila siku yoyote ile ikitokea naweza kuzaa. Sina sababu sijawapata nikipata nitakuwa nao. Sijaasili mtoto huyu mnayeniona naye ananiita shangazi, ninaishi naye kutokana na ukaribu wa shule anayosoma. Tunaishi wawili, anaitwa Makonyo Yvonne Mbibo ni binti wa mdogo wangu Dabo.

Sina mtoto niliyemuacha kijijini na sijawahi kuishi kijijini. Sijawahi kuishi Musoma, kwetu ni Bunda na huwa naenda ikitokea misiba kuzika, sijawahai kuishi huko hata zaidi ya miezi miwili. Nilizaliwa Shinyanga mjini na nilikuja Dar es Salaam nikiwa na miaka 11 na sijawahi kurudi huko tena zaidi ya kwenda kusalimia.

Swali: Mwanamume mwenye vigezo gani ungependa kuwa naye kwa sasa? Je kwa sasa unaye boyfriend?

Jibu: Anayejali na kujiheshimu, mwenye roho ya upendo na huruma anayeweza kuniangalia na kuniwezesha kifedha, asiyechepuka ovyo (milupo kila kona), asiwe tegemezi hata kama siyo tajiri lakini asinitegemee. Asiwe mlevi kupindukia wa kulala baa, wala kulala nje kwa machangudoa wa Kinondoni wa popote pale, nikikohoa tu awepo hapo. Nashindwa kutofautisha kati ya boyfriend na lover wanaojua kizungu wanaweza kunisaidia, ila kama ni kwa maana ya rafiki wa kawaida wa kiume ninaye na si pekee nina marafiki wengi sana wa kiume kuliko wa kike. Swali kuhusu ndoa nitalijibu Ijumaa (jana) na ndiyo litakuwa swali la mwisho.

Swali: Kama una ugomvi, utofauti na watu wasanii na wamiliki wa vituo vya redio, una mpango wa kupatana nao?

Jibu: Nitapatana na mtu atakayekubali kuwa alikosa, kama naamini yeye ndiye alinikosea itabidi aniombe msamaha. Kama mimi ndiyo nilimkosea nitaomba msamaha vinginevyo hakuna miujiza, siwezi kumwomba mtu msamaha endapo naamini kabisa sijamkosea, niliowahi kuwakosea nishawaomba msamaha wote hakuna binadamu asiyekosea ila siwezi kuongopa au kuwa na uoga wa maisha. Naamini hata niliuza nyanya bado wapo watu wanaohitaji nyanya na watanunua.

Swali: Kwa nini hufanyi kolabo na wasanii wa kike?

Jibu: Nimewahi kufanya na wasanii mbalimbali wa kike ila sijui kwa nini hamjazisikia. Mwasiti amewahi kunishirikisha, nimewahi kumwandikia na kushiriki kuimba kwenye wimbo wa Movement za Albino na K’Sher.

Nimemwandikia na kushiriki kwa Nakaaya Sumari. Nimewahi kumwandikia wimbo Patricia Hillary, nimeshirikisha Ray C kwenye wimbo wangu ‘Nimekubali’ kutoka albamu ya ‘Machozi’.

Pia wapo wasichana mbalimbali waliopitia Machozi Band na kujifunza kuimba leo mnawafahamu kumbukeni tu kuwa kutoka kwa mtu itategemea na nyimbo zake kutangazwa redioni na mimi siyo mwenye redio msaada pekee ni kushiriki kila ninapotakiwa kufanya hivyo.

Swali: Vipi kuhusu siasa ana mchango wako katika jamii?

Jibu: Siyo mpenzi na sitarajii kujihusisha na siasa, wala chama chochote. Kila binadamu ana mchango katika jamii kwa njia moja ama nyingine. Ukitambua moja lolote nililowahi kulifanya litakupa furaha ndiyo mchango wangu.

Swali: Kuhusu afya na urembo je, unapunguza mwili kwa mazoezi na kula? Nani anakupa vipodozi ‘make-up’ na nguo?

Jibu: Sifanyi diet nakula kuliko mwanamume, naweza kula kuku mzima kama chakula cha mchana ila kuna baadhi ya vyakula sili mfano, nguruwe, nyama nyekundu (ng’ombe, kondoo, mbuzi, swala nk). Nakula mboga mboga na vyakula vya wanga.