ANTIE BETTIE: Maumbile yake yamenishinda, nahisi anahitaji pete

Muktasari:

  • Anti nimefanya machejo yote ili nimudu haya maumbile ya mwenza wangu, lakini nimeshindwa. Nakiri nimeshindwa kujinafasi nikiwa faragha na mume wangu kutokana na ukubwa wa maumbile yake.

Anti habari! Nashukuru kwa kazi nzuri ya kutuelimisha tuliomo ndani ya ndoa na tunaotaka kuingia.

Naomba unisaidie kiungo cha uzazi cha mwanaume kikiwa nchi ngapi ndiyo anatakiwa kuvishwa pete, maana nimekuwa nikisikia kikiwa kikubwa kuna pete huwa wanavishwa ili kukipunguza. Nahisi mume wangu anatakiwa kupatiwa huduma hiyo kutokana na kuwa na kiungo kikubwa.

Ninampenda sana na ana sifa zote za kuwa mume wangu, lakini changamoto ni hicho kiungo kiasi kinaninyima raha, kila nikijitahidi kukizoea kama wengi wanavyonishauri ninashindwa. Antie hiki kiungo si cha kawaida na kinanizidi uwezo, nimefanya machejo yote imeshindikana. Ili niendelee kuwa naye kama moyo wangu unavyotaka natamani apatiwe hiyo huduma ya pete.

Au nishauri nifanyeje?

Pole na hongera, inawezekana hicho kiungo ni kikubwa kutokana na maumbile yako wewe, wapo wengine wakikipata ni saizi yao.

Anayeweza kuthibitisha kuwa mumeo anapaswa kuvishwa pete au laa ni daktari. Hivyo tumia ushawishi wako wa kike mwende hospitali na mumeo ukamueleze tatizo hilo daktari.

Akiwasikiliza ninyi nyote atakuwa na nafasi nzuri ya kumvisha pete au kuwapa ushauri. Wakati huu unapoendelea kumshauri kwenda hospitali badilisha mikao mnapokutana inawezekana unavyokaa ndiyo unaisikia kwa karibu zaidi.

Inakusumbua kwa sababu hujaijulia, ukiitafutia mbinu mbadala inawezekana aihitaji pete kama unavyodhani.

Muhimu na mumeo ajue kuwa maumbile yake yanakushinda ili akusaidie jinsi ya kukabiliana nayo na itakuwa rahisi hata kwenda naye hospitali.

Tafuta namna nzuri ya kumueleza, kama unaumia kwa maana ya kupata majeraha au michubuko muonyeshe kama ushahidi. Usisahau kumwambia kuwa mnapaswa kutafuta suluhisho na si vinginevyo. Asije kudhani unataka kumuacha au kutafuta mwingine bure.

Ila una bahati sana, wenzako weng wanalalamika kuikosa huduma hiyo adhimu.