Kula samaki kwa wingi kuondoa mikunjo usoni

Kula samaki kwa wingi kuondoa mikunjo usoni

Muktasari:

  • Licha ya kuwapo kwa vitu vingi vinavyosaidia kuboresha ngozi, yakiwamo matunda na mimea mbalimbali, pia kuna vyakula.

Licha ya kuwapo kwa vitu vingi vinavyosaidia kuboresha ngozi, yakiwamo matunda na mimea mbalimbali, pia kuna vyakula.

Miongoni mwa vyakula hivyo ni vya baharini, hapa namaanisha samaki wa aina zote, wakiwamo pweza ambao wengine huwatumia kwa malengo tofauti kidogo na haya.

Samaki wengi wana wingi wa madini ya zinc na omega 3 ambazo ni muhimu kwa usimamizi wa ngozi.

Omega 3 husaidia ngozi isikakamae, isiwe kavu na isikunjamane.

Pia husaidia mzunguko wa damu katika mwili kufanya kazi vizuri.

Hivi vitu vinapokuwa sawa mwilini, bila shaka kila kitu kinakuwa sawa.

Hivyo pamoja na kutumia vitu vingine kuboresha ngozi, jitahidi kula samaki wa aina mbalimbali ili kuipa ngozi mwonekano wa ujana muda wote.