Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Leyla ajigamba kuwa na ‘nywila’ ya mtima wa Mzee Yusuph

Muktasari:

Kwa mujibu wa msanii huyo, anampenda mumewe na kama binadamu anamuonea wivu, lakini anajiamini ndiyo maana hana wasiwasi akimuona na wanawake, kwa sababu anaamini wengi ni mashabiki wake na hata wale wanaomfuata kwa nia ya mapenzi hawatafanikiwa kwani namba ya siri ya kufungua moyo wa mkali huyo anayo yeye

Ana sura ya kuvutia, macho maangavu yanayovutia kumtizama, anazungumza taratibu lakini maneno yenye akili. Huyo ni Leyla Rashid mke halali wa mkurugenzi wa kundi la muziki wa miondoko yo taarabu la Jahazi Modern, Mzee Yusuph aliyebainisha kuwa licha ya mumewe kuwa na mashabiki wengi wa kike hana analopoteza kutoka kwake.

Kwa mujibu wa msanii huyo, anampenda mumewe na kama binadamu anamuonea wivu, lakini anajiamini ndiyo maana hana wasiwasi akimuona na wanawake, kwa sababu anaamini wengi ni mashabiki wake na hata wale wanaomfuata kwa nia ya mapenzi hawatafanikiwa kwani namba ya siri ya kufungua moyo wa mkali huyo anayo yeye.

Anabainisha kuwa hata siku moja hajawahi kukutana na kadhia ya wanawake kumtongoza mumewe ila anahisi wapo wanaofanya hivyo na kwamba haumizi kichwa kwa sababu hawawezi kufungua uvungu wa moyo wa mkali huyo wa nyimbo za mapenzi kwa sababu yeye ndiyo ufunguo na kama ni namba ya siri ya kufungulia bado anayo yeye.

“Ukijiamini unapendwa raha sana, hata ukimkuta mumeo na mtu huna papara kwa sababu kama hakusema anatakwa basi hatofanya kitu kibaya, nina raha na amani ya moyo,” alisema Leyla.

Leyla alikiri kuwa mumewe ana marafiki wengi wa kike kwa sababu ya uimbaji wake na kwamna wanawake wengi wanavutiwa na kazi zake, hivyo hajawahi kulalamika wala kuumia roho akimuona nao.

Ndoa na kazi

Anajigamba kuwa anamudu kufanya yale muhimu yanayohitajika kwenye ndoa kwa sababu anajipangia muda wa kuwa na m familia na kuwa katika kumbi za starehe kuburudisha mashabiki wao.

Leyla ambaye pia ni mwimbaji katika bendi ya mumewe, anajinasibu kuwa kama mke lazima ampikie mumewe na iwapo hatapata nafasi ya kufanya hivyo kutokana na uchovu au kazi nyingi basi humuomba ridhaa yake akikataa hata saa sita usiku humpikia.

“Kama mumeo anakula chakula cha kuandaliwa na msaidizi kiasi kwamba siku ukipika mwenyewe anatambua na kulalama chakula kibaya hakuna haja ya kuwapo na kujisifu umeolewa, naacha kazi nafanya kazi ninapoingia jikoni kumpikia mfalme ili siku akila chakula kilichopikwa na mtu mwingine atamani kula nilichopika mmiliki halali,” alisema Leyla.

Alifafanua kuwa anafanya yote hayo kwa sababu anampenda Mfalme Mzee Yusuph na analipa mapenzi anayopewa na mumewe huyo.

“Mfalme anajua kupenda na maana yake, kwani ukiwa naye ni kata kiu tosha, siyo kwa mazungumzo kama mume lakini kwa uongozi kama baba wa familia, anampenda na kumheshimu kila mmoja, lakini akinipenda zaidi na kuonyesha wazi kuwa ananipenda,” alisema Leyla huku anacheka.