Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Usikubali kuoa au kuolewa kwa sababu ya huruma

Picha na Mtandao.

Kuna kisa tunachokijua fika tulichohusika kusuluhisha kinafikirisha. Kuna jamaa yetu (jina hatutaji), aliamua kuoa kwa kumhurumia mwingine kiasi cha kujiumiza.

Akiwa chuoni, jamaa huyu mtanashati, aliyejaliwa akili zinazochemka na sura ya kupendeza, alikutana na mwanachuo mwenzake wa kike.

Wawili hawa, kama watu wengine, walizoea kuonana chuoni. Hakuna aliyemchukulia mwenziwe kwa upekee zaidi ya kuwa wanachuo. Siku moja, rafiki yake alimtambulisha kwa mwanafunzi wa kike.

Binti huyu hakujaaliwa sura nzuri. Alikuwa yupo yupo tu. Isitoshe, umri ulikuwa umeanza kwenda. Ambacho jamaa hakujua ni kwamba yule binti alikuwa kiumbe katili na mwenye mambo mengi mabaya na sio sura tu.

Baada ya kutambulishwa, binti aliona ajaribu bahati yake. Kila mara akikutana na jamaa, humsalimia kwa heshima. Hata hivyo, Jamaa hakushuku lolote zaidi ya kuendelea na masomo yake.

Binti alianza taratibu kupita kila alipokuwa jamaa na kumsalimia. Alimpeleleza akajua anakosomea na kuhamia kule angalau awe karibu akimtupia jicho. Jamaa hakuonyesha kujali.

Baada ya miezi kadhaa kupita bila kuona lolote la kuweza kuanzisha uhusiano. Pamoja na sura yake nzuri, akili, na utanashati, unaweza kumuita ‘innocent’ kwa maana ya neno. Binti alivutiwa sana na uzuri wa jamaa huyu, ila nafsini mwake, hakuamini yule jamaa angemfikiria achilia mbali kumpenda.

Muda ulizidi kuyoyoma huku binti akiongeza juhudi katika mawindo yake. Kila akimuona yule jamaa, huenda kumsalimia kama kawaida yake.

Kadri siku zilivyozidi kwenda, binti alizidisha ukaribu hadi akagundua. Kumbe kijana wa watu hakuwa kwenye uhusiano wowote na hakuwa uzoefu katika uhusiano. Hivyo, alipiga moyo konde kumuandama.

Bila hili wala lile, siku moja, binti akamuomba yule kijana msaada. Kijana alimsaidia akijua ni msaada mdogo tu wa kimasomo asijue alikuwa anaingia kwenye nyavu za shetani. Baadaye walikuna wakakaa meza moja kwenye bustani ya chuo. Binti alikuja kaupara kweli kweli. Kijana hakuwazia lolote. Alingoja kusikia yule binti alikuwa akitaka msaada gani.

Baada ya kukaa mezani, yule binti alifungua moyo. Alimueleza kuwa alitoka familia maskini. Jamaa alimuonea huruma na kumpa moyo asome amalize apate kazi nzuri aikomboe familia yake.

Maongezi yaliendelea. Yule binti akamwambia kuwa alikuwa na mchumba aliyeuawa kikatili bila kueleza kisa na sababu. Yule jamaa ilimjia huruma akampa pole na kumtia moyo kuwa angepata Mungu aliyempangia.

Siku hiyo, alimpa yule binti fedha kadhaa zikamsaidie na kwenda zake. Baada ya wiki moja, yule binti alirejea na barua yenye shukrani akamkabidhi yule kijana.

Kwa vile yule kijana hakujua dhamira ya binti yule, aliipokea, kuisoma, na kufurahi. Baada ya muda, binti alimuomba, kama ingemfurahisha, waende wote kwenye chumba alichokuwa akiishi. Kijana hakupinga. Walipanga siku ya kufanya hivyo.

Siku ilipofika, binti aliupara kama kawaida yake. Alikwenda kwenye idara ya yule kijana na kumtafuta tayari waende. Kijana alimpokea kama kawaida. Waliamua waondoke kwenda kupanda basi. Yule kijana alisema alikuwa na gari lake. Hivyo, hawakuhitaji basi.

Kugundua kijana alikuwa na gari, binti alidhamiria zaidi. Walipofika nyumbani, bibi akamwambia kuwa alikuwa akimpenda kuliko chochote duniani. Kijana alichanganyikiwa.

Haukupita muda, binti akamwambia kuwa ameona kuwa yeye ndiye Mungu aliyemchagulia. Kijana hakuamini masikio yake. Ila alifanya kosa moja. Aliamua kukmuonea huruma na kumridhisha kwa kujipa moyo kuwa wanaweza kuwa na uhusiano wa muda. Siku hiyo binti alijirahisi hadi wakalala. Mtego ulikuwa umenasa.

Taratibu, kijana akanogewa na kunasa jumla. Binti alitegeshea mimba na kusema asingemuoa wazazi wake wangemuua. Kijana alivuta kitu ndani maisha yakaanza kwa upendo na raha.

Mwisho ndoa ilivunjika baada ya kijana kugundua kuwa yule binti alikuwa ni kahaba mwenye uwezo wa kutembea hata na nduguze.

Hii ilimhuzunisha mume akakumbuka alivyoingizwa mtegoni tena na kiumbe mwenye sura na tabia mbaya. Mwisho wa yote, huruma yake ilivyoponza akaishia kuacha na kujuta kabla ya kuharibu maisha yake jumla. Je, haya hayapo/

Somo: usioe au kuolewa kwa kumhurumia mtu bali kwa kumpenda na kumchunguza uone kama anakufaa na siyo kumhurumia. Majuto ni mjukuu. Tieni akilini watarajiwa kwenye ndoa.