Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanaume wa kisasa wana ‘umama’ kidogo

Muktasari:

  • Kwa mfano kwenye usiri, unakuta mwanaume ana nyumba ndogo yake, lakini ana uwezo wa kudumu nayo miaka nenda rudi na mke asigundue chochote. Na sio kudumu nayo tu, hadi watoto wakazaa lakini familia huku nyumbani isielewe ng’o. Utashangaa tu, siku mzee akikata roho watoto wanaibuka kutoka kusikojulikana kuja kudai mirathi iliyoachwa na baba yao.

Wanaume siku hizi tumebadilika sana, tumepoteza kabisa zile tabia zetu za asili, tabia halisi. Zamani, enzi za wazee wetu, wanaume walikuwa na misimamo, hawakuwa waoga na walikuwa wasiri mno.

Kwa mfano kwenye usiri, unakuta mwanaume ana nyumba ndogo yake, lakini ana uwezo wa kudumu nayo miaka nenda rudi na mke asigundue chochote. Na sio kudumu nayo tu, hadi watoto wakazaa lakini familia huku nyumbani isielewe ng’o. Utashangaa tu, siku mzee akikata roho watoto wanaibuka kutoka kusikojulikana kuja kudai mirathi iliyoachwa na baba yao.

Na hapo inakuwa ngumu sana kukubalika hasa na mke wa marehemu kwa sababu yeye kama mke alikuwa akiziamini sana nyendo za mume wake; kwa mfano mzee alikuwa anarudi mapema nyumbani, saa kumi na mbili yuko sebuleni anaangalia ‘Jiji Letu’, sasa huo muda wa kukutana na ‘mchepuko’ hadi wakazaa na watoto alikuwa anaupata wapi? Na isitoshe, licha ya kuwa na michepuko wazee wetu walikuwa wanajua kuigiza bwana, yaani hata mchepuko awe na jitihada za namna gani huko nje, lakini wazee walikuwa hawabadiliki tabia kwa wake zao, mtu anakuwa na tabia zilezile za tangu wanaoana; haleti dharau wala maneno ya hovyo kwa mke wake.

Ila wanaume wa siku hizi tumekuwa changamoto sana, hatuna chochote kinachotufananisha na wazee wetu. Waoga, hatuna misimamo na sio wasiri kabisa.

Siku hizi tukipata kamchepuko tu hata mwezi hauishi mke anaweza kugundua. Na imekuwa rahisi sana kwa sababu hatuna misimamo. Unaweza kutoka zako kazini ukaona ngoja upite kwanza kwa mpango wa kando, upumzishe akili kisha mapema utarudi nyumbani. Lakini ukifika huko, mchepuko anakupangia ratiba zake za ajabu ajabu na wewe kwa sababu ya kutokuwa na msimamo unaamua kuzifuata na matokeo yake unapiga simu nyumbani, unadanganya una kikao ofisi, utachelewa kurudi—huu ni udhaifu aisee.

Au wengine tukipata vipozeo huko nje tunabadilika kabisa tabia, tunakuwa na hasira za hovyo hovyo kama wajawazito bwana. Mke akishika simu yako kidogo unafoka, unataka na kumbamanda na makofi kabisa.

Nakwambia michepuko ya enzi hizi imekuwa na kazi rahisi sana kwa sababu imetukuta wanaume wenyewe tuna ‘umama’ kidogo—uwoga, kutokuwa na msimamo na kushindwa kutunza siri hizi zote ni tabia zinazowapendeza wanawake na mwanaume kuwa na tabia ni kuwa na umama.

Mwanaume kupelekwa pelekwa na mchepuko kama sio umama ni nini? Wanawake siku hizi hawatuogopi na hawana heshima kwa wake zetu kwasababu tumewaruhusu watutawale. Tumewaonyesha udhaifu wetu.

Mwanamke anaanzaje sasa kukuzuia usipokee simu ya mkeo au uondoke muda anaotaka yeye?