Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bilioni 15 za taasisi ya Aga Khan zinavyoboresha elimu mikoa ya Kusini

Meneja mradi wa SESEA, Ronald Kimambo akizungumza na wanahabari. Picha na Hadija Jumanne

Muktasari:

Shuleni hali siyo shwari, kwani kumekuwapo na taarifa zinazoonyesha idadi kubwa ya wanafunzi wanaomaliza ya elimu ya msingi wakikosa stadi muhimu za kusoma na kuandika.

Hadi kufikia mwaka 2002 idadi ya watu wasiojua kusoma na kuandika nchini ilikuwa watu 6.2 milioni, idadi hiyo ni kwa watu wenye umri wa miaka 15 na kuendelea.

Hali ya kutojua kusoma na kuandika haiko tu kwa watu wazima, bali hata kwa wanafunzi wadogo.

Shuleni hali siyo shwari, kwani kumekuwapo na taarifa zinazoonyesha idadi kubwa ya wanafunzi wanaomaliza ya elimu ya msingi wakikosa stadi muhimu za kusoma na kuandika.

Kwa mfano, mwaka 2012, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, ilibaini kuwapo kwa wanafunzi 5,200 walioingia sekondari wakiwa hawajui kusoma na kuandika.

Uzoefu unaonyesha kuwa wanafunzi wengi wanakosa msingi wa masomo hayo tangu wakiwa elimu ya awali na madarasa ya mwanzo ya elimu ya msingi (darasa la kwanza hadi la tatu).

Mradi wa SESEA

Kutokana na ukubwa wa tatizo hilo, Chuo Kikuu cha Aga Khan na Taasisi ya Maendeleo ya Elimu ya chuo hicho (AKU-IED) kupitia mradi wake SESEA, wameanzisha mradi wa kuimarisha mifumo ya utoaji elimu unaolenga zaidi katika katika uimarishaji wa mafunzo ya stadi za kusoma na kuandika

Huu ni mradi wa kuimarisha mifumo ya elimu katika kanda ya Afrika Mashiriki na unatekelezwa katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda.

Meneja Mradi wa SESEA, Ronald Kimambo anasema mradi huo ni wa miaka mitano ulioanza Aprili 2013 na kutarajia kukamilika Desemba 2017.

Kwa Tanzania mradi huo unatekelezwa mikoa ya Kusini katika Wilaya ya Nachingwea ikihusisha Chuo cha Ualimu Nachingwea, Newala ikihusisha Chuo cha Ualimu Kitangali. Maeneo mengine ni Kilwa na Lindi.

“Mradi huo una malengo matatu ambayo ni kutoa mafunzo kwa walimu, kuboresha mifumo ya elimu na kufanya utafiti na midahalo,” anasema Kimambo.

Anasema katika kipindi cha miaka miwili iliyopita wamefanikiwa kutoa mafunzo kwa watu 371 wakiwamo walimu wa shule za awali na msingi, maofisa wa elimu na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu katika mikoa hiyo.

Kuhusu faida za mradi hadi sasa, anasema: “Idadi ya watoto wanaojiunga na elimu ya awali imeongezeka katika maeneo yenye mradi huo, kutokana na walimu kupatiwa mafunzo ya kuimarisha ufundishaji wa walimu wa elimu ya awali na shule za msingi.’’

Kauli ya Serikali

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, Lameck Chota, anasema mradi huo umewezesha kuongezeka kwa usajili wa watoto wanaoandikishwa elimu ya awali hadi kufikia asilimia 78, huku wanaojiunga na darasa la kwanza wakifikia asilimia 91.

Pia anasema wamefanikiwa kuongeza kiwango cha ufaulu kwa shule za msingi hadi kufikia asilimia 60 mwaka 2014, huku ikishika nafasi ya pili kimkoa kwa kupata asilimia 50.

“SESEA imechangia katika kuyafikia malengo ya Dira ya Taifa ya mwaka 2015, ambayo lengo lake kuu ni kuwa na jamii yenye maendeleo makubwa na watu wenye viwango bora vya kujikimu kimaisha,”anasema.

Moja ya shughuli inayofanywa na SESEA ni kutoa mafunzo kazini kwa walimu kupitia kozi za ngazi ya cheti na kozi fupi kwa walimu wa elimu ya awali na elimu ya msingi.

“Lengo la SESEA ni kujikita katika kuimarisha matokeo ya kujifunza katika ngazi za elimu ya awali na elimu ya msingi na kutoa kipaumbele kwenye mpango wa Serikali wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), katika kuboresha uwezo wa watoto kusoma, kuandika na kuhesabu wanapofikia darasa la pili,” anasema Mkuu wa idara ya programu za masomo wa Chuo Kikuu cha Aga Khan, Dk Geoff Tennant.

Mkoa wa Lindi

Kwa Mkoa wa Lindi, hali siyo ya kuvutia, kwani ripoti moja ya mradi huo umebaini kuwa zaidi ya asilimia 80 ya watoto wenye umri wa miaka mitatu hadi nane wanasoma katika mazingira magumu.

Ripoti hiyo iliyozinduliwa Novemba 2014, imeonyesha kuwa wanafunzi hao wanasoma katika mazingira magumu hasa wenye ulemavu wa viungo na wasioona.

“Tumegundua kuwa watoto wanashindwa kumudu kusoma, kuandika na kuhesabu kutokana na kukosa mazingira rafiki wanapokuwa shuleni na wanaporudi kwa wazazi,” anasema mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Agha Khan, Profesa Marriote Ngwaru.