Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hizi ndizo sifa za mwalimu bora- 1

Rajab Kipango

Muktasari:

Kwa jumla walimu wetu wametutoa mbali hadi tukafika hapa tulipo. Kule kujua kusoma na kuandika tu ni mchango mkubwa wa walimu, achilia mbali wale waliofanikiwa kusoma hadi ngazi za juu.

Ualimu ni mojawapo ya fani muhimu kwa maendeleo ya taifa lolote lile duniani. Kila mmoja wetu anatambua umuhimu na michango ya walimu katika maisha yake ya kila siku.

Kwa jumla walimu wetu wametutoa mbali hadi tukafika hapa tulipo. Kule kujua kusoma na kuandika tu ni mchango mkubwa wa walimu, achilia mbali wale waliofanikiwa kusoma hadi ngazi za juu.

Walimu wetu hawa, hasa wa shule za msingi na sekondari, ndio waliotujengea msingi imara ambao umewawezesha baadhi ya watu kufika mbali kielimu na kimaisha.

Makala yetu haya naangazia sifa anazotakiwa kuwa nazo mwalimu, ambazo kimsingi zinamtofautisha mwalimu mwenye weledi na mwalimu kanjanja.

Kwa mwalimu yeyote ambaye amesomea kazi hii ya ualimu, atakuwa anajua baadhi ya sifa hizi nitakazozungumzia, kwani wakufunzi wengi makini daima huwafundisha walimu wanafunzi sifa hizi ili kuwaandaa kimaadili na kuwa walimu bora.

Lakini kwa kuwa lengo la makala hii si kuwafikia walimu pekee tunalazimika kuziandika ili jamii kwa jumla iweze kuzifahamu, ili wawe makini katika kufanya uamuzi wapi wapeleke watoto wao kuelimika.

Maadili mema na kujiheshimu ni sifa mojawapo kubwa ya mwalimu bora. Mwalimu anatakiwa atambue kuwa yeye ni kigezo kwa wanafunzi wake, hivyo anatakiwa ajiepushe na mambo yatakayomjengea taswira mbaya kwa wanafunzi wake na jamii kwa jumla.

Mwalimu bora na makini anatakiwa ajiepushe na tabia mbaya kama ulevi na uzinzi. Inashangaza katika zama tulizonazo kuona mwalimu aliyekabidhiwa jukumu la malezi ya watoto, anafikia hatua ya kutembea na wanafunzi wake hata kufikia kuwapa mimba

Hii ni dhambi isiyosameheka hata kidogo. Hivi inakuwaje jamii imekuamini kiasi cha kukukabidhi watoto wao uwaelimishe halafu wewe unafanya hiyana kama hii? Hii ni sawa na kutafuna kondoo uliokabidhiwa kuwachunga.

Ubunifu darasani ni sifa nyingine kubwa anayotakiwa kuwa nayo mwalimu. Angalia kwanini baadhi ya wanafunzi wako wanakuwa wagumu kuelewa darasani na njoo na mbinu mbadala zitakazoleta mabadiliko darasani.

Usiwe mtu wa kukariri tu bali jitahidi kusoma kutoka kwenye vyanzo mbalimbali, ili uweze kuboresha maarifa yako. Baadhi ya walimu hawajiandai kwa ajili ya somo.

Wengine maelezo aliyofundishia miaka ishirini iliyopita ndiyo hayohayo anayofundishia leo, japokuwa yanaweza kuwa yamepitwa na wakati.

Tuache tabia ya kanyaga twende darasani bali tuwasaidie wanafunzi hasa wale wenye uelewa taratibu ili waweze kwenda na kasi ya wenzao darasani.

Kuwajali na kuwathamini wanafunzi wako ni sifa muhimu kuwa nayo kama mwalimu. Wapende na wajali wanafunzi wako na jitume kuhakikisha kuwa wanafaulu katika masomo yao.

Jambo la kushangaza katika taasisi za elimu ya juu, baadhi ya walimu hujitapa kwamba safari hii ‘wamekamata’ (kufelisha) wanafunzi kadhaa kwenye mtihani yao!

Katika chuo kimoja nilichosoma, mwalimu mmoja alikuwa hafichi kuwaambia wanfunzi wake kuwa safari hii nitakamata nusu ya darasa.

Badala ya kusikitika kwamba kufeli kwa wanafunzi husika kunaakisi moja kwa moja upungufu wake kama mwalimu, yeye aliona fahari! Hii ni sifa isiyofaa kwa mwalimu.

Kuwa na huruma kwa wanafunzi ni sifa muhimu kuwa nayo mwalimu. Tambua kuwa wanafunzi wako wanaweza kuwa na matatizo kifamilia na hata kiuchumi na uwe tayari kuwasaidia kiushauri ili wasiathirike kimasomo.

Itendelea