Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shamsa Ford: Nakomaa na ndoa mpaka kieleweke

Ndoa nyingi huyumba miaka ya mwanzo hasa pale ‘inapochelewa kujibu’. Kwa mwigizaji Shamsa Ford ambaye sasa ameanza safari ya kuutafuta mwaka wa tatu ni tofauti.

Ameeleza namna familia ya mume wake, Chid Mapenzi, inavyomchukulia licha ya kuchelewa kumzalia mtoto.

Chid na Shamsa walifunga ndoa Septemba 2, 2016 na mpaka sasa haijajibu, japokuwa Shamsa ana mtoto aliyezaa na mwanaume mwingine kabla hajaolewa.

Katika mahojiano yake na Mwananchi, Shamsa ambaye aliitendea vyema filamu ya Chausiku, amesema anashukuru pamoja na kuchelewa kupata mtoto, ndugu wa mume hawajawahi kumsimanga kwa maneno kama inavyokuwa kwa wanawake wengine.

Anasema, “Kwa kweli nashukuru nimepata wakwe na mawifi wastaarabu maana kweli ingekuwa familia nyingine kwa muda niliokaa na mtoto wao wangeanza kunisema vibaya, lakini kwa ndugu wa Chid wala halijanitokea hilo.”

“Nadhani linapofika suala la watu kupata mtoto jamii inapaswa kujua kwamba ni mipango ya Mungu na wakati mwingine huenda hata wahusika wenyewe hawajaamua, hauwezi kuwalazimisha.”

Pamoja na hayo anakiri kwamba anatamani amzalie mumewe huyo ambaye ni mfanyabiashara maarufu wa mavazi.

Kuhusu anavyoona maisha ya ndoa, Shamsa anasema kwake ni poa tu na kueleza kwamba anashukuru mume aliyempata ni mwelewa na wamekuwa wakisikilizana katika mambo mengi. Wakati kuhusiana na sakata lake la kupigwa mara kwa mara na mwanaume huyo, Shamsa alisema hilo lilimtokea mara moja na ilisababishwa na yeye kupaniki pale Chid alivyomtania kumpiga na yeye kuchukulia kama kweli.

“Mwenzangu alikuwa anatania kama mtu anayetaka kunipiga, lakini mimi nikachukulia kuwa yupo serious, kumbe sivyo na katika purukushani za kumrudishia basi bahati mbaya ndio hivyo akajikuta ananijeruhi, lakini sio mwanaume mwenye tabia hizo za kupiga,” anasema.