Makocha wazawa walivyogaragazwa Afcon 2017

Basiro Cande

Muktasari:

Safari hii, makocha wote wanne waliokuwa wazawa, timu zao zimeondoshwa kwenye fainali hizo mapema.

Kwa mara ya 16 katika historia ya Kombe la Mataifa ya Afrika, makocha wa kigeni wanaendelea kutawala wakati makocha wazawa wakionekana si mali kitu katika fainali hizo.

Safari hii, makocha wote wanne waliokuwa wazawa, timu zao zimeondoshwa kwenye fainali hizo mapema.

Makocha wazawa waliojitutumua walikuwa wa Senegal na DR Congo, waliofikisha timu zao robo fainali, waligawana wikiendi iliyopita, Senegal, Simba wa Terranga iliyokuwa chini ya nahodha wake wa zamani, Aliou Cisse ilipotea kwa Hugo Broos anayeinoa Cameroon ‘Simba Wasiofugika’.

Jumapili iliyofuata, DR Congo iliyokuwa ikinolewa na Florent Ibenge ilimwagwa na Ghana ‘Black Stars’ inayofundishwa na Muisrael, Avram Grant.

Baada ya robo fainali, wakabakia makocha wanne wa kigeni, Hector Cuper (Argentina) ambaye ni raia wa nje ya Bara la Ulaya, Paul Duarte (Burkina Faso) ni raia wa Ureno.

Pamoja na hayo, katika fainali za mwaka huu, kulikuwa na makocha wanne tu wazawa nchini Gabon katika fainali hizo za 31.

Timu zilizokuwa na wazawa mbali na Senegal na DR Congo ni Guinea Bissau (Baciro Cande) na Callisto Pasuwa (Zimbabwe) ambao timu zao ziliaga hatua ya makundi. Mpaka sasa, mataji 16 kati ya mashindano 31 yametwaliwa na wageni ikiwamo fainali ya jana ambayo Cameroon ilikuwa chini ya Hugo Broos (Ubelgiji) na Hector Cuper (Argentina) anayeinoa Misri.

 

Makocha wazawa

Kocha wa mwisho mzawa, marehemu Stephen Keshi aliiwezesha Nigeria ‘Super Eagles’ kutwaa ubingwa mwaka 2013.

Itakumbukwa Keshi aliwahi kusema kuwa mataifa ya Afrika yana hazina ya watu wao, hivyo hakuna sababu ya kuchukua makocha wa kigeni.

Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Malawi, Kinnah Phiria aliwahi kupaza sauti katika hili: “Kwangu mimi, nadhani hii imejengeneka kwenye akili zetu kama Waafrika kwamba hatuwaamini watu wetu.”

Mkongwe wa soka Zambia Kalusha Bwalya alisema: “Ninadhani mataifa ya Afrika lazima kuwaamini watu wao, wapewe mafunzo na kikubwa ni uvumilivu katika kusimamia majukumu ya timu ya taifa.”

Wakati Bwalya akisema hayo, inaelezwa kuwa idadi ya makocha wa kigeni imeongezeka ikilinganisha na mwaka 2015 wakati huo kulikuwa na kocha mmoja.

Ilikuwa mapema mno lakini baada ya mechi za raundi ya kwanza, walianza kuachana kwani mechi sita zilichezwa na kati ya hizo, mbili za ushindi walikuwa makocha wazawa.

Cisse akiwa na Senegal aliifunga Tunisia inayonolewa na Henryk Kasperczak wa Poland mjini Franceville wakati Florent Ibenge wa DRC aliifunga Morocco bao 1-0 chini ya Herve Renard mjini Oyem.

 

Uwezeshwaji

Kwa kupata mahitaji muhimu na kuungwa mkono kwa wazawa mafanikio yanaweza kuwepo kama ilivyokuwa kwa Keshi kuwa mzawa wa kwanza Nigeria, Wanne Afrika Magharibi na kocha wa 11 kutweaa ubingwa wa Afrika baada ya Nigeria kuilaza Burkina Faso katika fainali mwaka 2013.

Pia mwaka 1994 alishinda kama mchezaji wakati Nigeria ilipoitoa nishai Zambia katika fainali.

Makocha Mourah Fahmy, Ydnekatchew Tessema, Charles Gyamfi na Hassan Shehata ni makocha wazawa waliowezesha nchi zao kutwaa ubingwa.

Gyamfi ni kocha mwenye mafanikio Ghana kwa aliiwezesha kutwaa ubingwa mwaka 1963 na 1965.