Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

UCHAMBUZI: Namna tiba mbadala zinavyoweza kusaidia viwanda

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu

Muktasari:

Hivyo basi, namna nzuri ya kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli yenye lengo la kukuza uchumi wa Taifa letu ni kila mtu afanye kazi, mamlaka za umma nazo zisaidie kutambua vyanzo vidogo vya uzalishaji ambavyo vinaweza kuchangia kuongeza kasi ya kukuza uchumi na ajira badala ya kuangalia vyanzo vikubwa pekee.

Tanzania ya viwanda kama inavyonadiwa na Rais John Magufuli inawezekana kwa namna nyingi, ikiwamo eneo la tiba mbadala.

Hivyo basi, namna nzuri ya kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli yenye lengo la kukuza uchumi wa Taifa letu ni kila mtu afanye kazi, mamlaka za umma nazo zisaidie kutambua vyanzo vidogo vya uzalishaji ambavyo vinaweza kuchangia kuongeza kasi ya kukuza uchumi na ajira badala ya kuangalia vyanzo vikubwa pekee.

Kaulimbiu ya ‘Hapa Kazi tu’ inasisitiza ujenzi wa Tanzania ya viwanda ambayo watalaamu wa tiba asili hatuna budi kuiunga mkono kwa kuwa wabunifu wa tiba zitakazosaidia kujenga afya bora ya Watanzania ili washiriki vizuri katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.

Watanzania tunapaswa kuiga nchi zilizonufaika na dawa za asili katika ujenzi wa uchumi. China ni moja ya nchi zilizofaidika na tiba asili ambayo inachangia Pato la Taifa kwa wastani wa Dola 15 bilioni za Marekani kwa mwaka nasi tunaweza pia. Isitoshe Tanzania ina mimea-dawa mingi inayofanya kazi vizuri kuliko China.

Iwapo watalaamu wa dawa za asili watafanya ubunifu wa kuanzisha viwanda vya dawa kama ilivyo China, India na nchi zingine za Asia, Pato la Taifa litaongezeka na afya za Watanzania kuimarika.

Naamini soko la tiba mbadala litakuwa kubwa kwa nchi nyingine za Afrika kwa kuwa hazina mimea tiba mingi kama ilivyo kwa Tanzania. Kinachotakiwa ni kuchukua hatua stahiki.

Watalaamu wa tiba za asili tuliwahi kufanya kikao kilichowahusisha Shirikisho la Vyama vya Tiba Asili (Shivyatiata) na Waziri wa Afya kuzungumzia uendelezaji wa tiba na namna tamko la kufuta vibali vya matangazo ya dawa na tiba za asili lilivyoathiri wadau.

Sekta ya tiba asili inaweza kufanikisha kuifikia azma ya Rais Magufuli ya kuipata Tanzania ya viwanda kwa kutekeleza agizo la Waziri wa Afya la kufuata sheria na kanuni za tiba asili wakati wa kutangaza huduma hizi.

Malengo ya watoa tiba hizi ni kufanya uwekezaji kwenye mimea-dawa na tayari fomula ya dawa imeshaandaliwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali zikiwamo serikali za vijiji na zaidi ya wakulima 50,000 wamekubali kulima mimea inayohitajika kwa uzalishaji wa dawa hizo.

Pamoja na yote hayo, tunampongeza Waziri wa Afya, Baraza na Sekretariati ya Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala kwa kuzindua fomu ya usajili wa dawa za asili. Hii ni hatua nzuri na kubwa kwa sababu itarasmisha dawa zetu ili ziweze kutambulika.

Pamoja na makusudi mazuri ya fomu ya usajili, kuna tatizo kwa Serikali ambayo bado haijatoa ruhusa ya matangazo ya huduma za tiba mbadala ambayo licha ya kusubiri kwa muda mrefu, msisitizo unaotolewa ni kwamba dawa husika inapaswa iwe imesajiliwa ndipo itapata kibali cha matangazo.

Ombi kwa Rais Magufuli na Waziri wa Afya, mtupe ruhusa sisi matabibu ambao tumekuwa kwenye tiba asili, tuendelee kutangaza huduma zetu za dawa asili kulingana na sheria namba 23 ya mwaka 2002, wakati tukitekeleza hatua za usajili wa dawa katika kipindi cha miaka mitatu. Na watakao shindwa kutekeleza usajili ndani ya kipindi hicho, matangazo yao yasimamishwe.

Tunaomba ruhusa ya matangazo ya dawa zetu za kiasili kwa sababu sera ya afya bado haijaruhusu dawa za asili kupatikana hospitalini, maduka ya dawa na kulipiwa kwa bima. Kwa kufanya hivyo kutatuweza kuanza uwekezaji wa viwanda vya dawa za asili.

Mwandishi ni mtaalamu wa tiba za asili na anapatikana kwa namba 0767700900