Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Madiwani wakasirika kuvalishwa majoho machafu

Madiwani wa manispaa ya Shinyanga wakivaa majoho tayari kwa kula kiapo cha uaminifu. PICHA| MALUNDE1 BLOG

Muktasari:

  • Sengerema alisema kwa mwaka majoho hayo hutengewa Sh1.2 milioni kwa ajili kuyafua, lakini wanashindwa kuelewa namna fedha hizo zinavyotumika.

Shinyanga.  Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, wamemjia juu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo wakidai kupewa majoho machafu yanayotoa harufu.

Madiwani hao walihoji kutaka kujua bajeti inayotengwa kwa ajili ya kufua majoho hayo.

Akizungumza kwenye kikao  cha kupitisha Bajeti ya mwaka 2017/18 juzi, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Isaack Sengerema ambaye pia ni Diwani wa Iselamagazi, alisema inasikitisha kupewa majoho yananuka ilhali bajeti ya kuyafua inatengwa.

Sengerema alisema kwa mwaka majoho hayo hutengewa Sh1.2 milioni kwa ajili kuyafua, lakini wanashindwa kuelewa namna fedha hizo zinavyotumika.

Diwani wa Bukene, Luhende Majaliwa alisema ni bora bei halisi ya kufua joho ikawekwa wazi ili kujua lilipo tatizo, kutokana na udhaifu uliojitokeza kwani kitendo hicho kimewasikitisha.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Ngassa Mboje alisema majoho hayo yana muda mrefu, hivyo uangaliwe uwezekano wa kutafuta mengine.