Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

FYATU MFYATUZI: na kutengua aliyetaka kunizidi kete!

Katika chata letu kuna siri kali. M/kiti ni rahisi, kila kitu. Ni muungu unaopaswa kuabudiwa na kusifiwa hata unapoboronga au kukosea. Ukiwa M/kiti, unaweza kumteua umtakaye akuhusu au asikuhusu, awe mshikaji, mshirika, mkeo, mkweo, shemeji au mumeo na usivunje sheria.

Katika kufaidi na kutumia umungu mtu na utukufu wangu, juzi nikamteua na kutengua kidhabi limbukeni, mjivuni, msanii na msakatonge kuwa katibu wa danganya toto na rongorongo wa chata. Huyu ni yule aliyeibuliwa na mtangulizi wangu toka jalalani.

Baadaye walikosana akapotea hadi juzi nilipomfufua nisijue la kufa halisikii dawa na la kuvunda halisikii ubani.

Najuta. Nilifanya kosa kumfufua, kumteua, kumuacha akaniudhi, kunitumia, kunichafua, na kunigeuza kituko na ngazi ya kupandia. Baada ya kugundua hila zake, nikamtumbulia mbali kulaleki.

Kweli, mwanaharamu ni mwanaharamu. Ukimuweka kwenye chupa, atatoa kidole. Huyu kwa upofu wake, alidhani nilimwibua ili kufyatua mafyatu wenzake wa kanda yake. Hivyo, nisingeweza kumfyatua.

Kumteua tu, aliona fursa kutaka kufanya alichomfanyia aliyemuumba. Alianza kutoa matamko ya nguvu kana kwamba ndiye M/kiti. Alipayuka na kujidai hata kuingilia mamlaka ya wenzake wanaomzidi vyeo akiwapigia simu, kuwaanika hadharani akitoa maagizo ya ajabuajabu bila aibu.

Alituchonganisha kwelikweli. Siri kali haiendeshwi majukwaani na kwa rukono. Hata hivyo, simshangai tokana na tamaa ya mamlaka na ukihiyo wake. Badala ya kutangaza chata, alijitangaza akidhani hajulikani janja yake.

Badala ya kueneza itakadi ya chata, alijieneza na itikadi zake uchwara akidhani siku moja atakuwa rahisi wa mafyatu ning’atukapo. Thubutu!

Badala ya kujenga chata, alilibomoa kwa kujijenga binafsi tena kwa kunibomoa na kufanya nionekane mbaya na asiyefaa. Alifanya mambo yaliyonitia aibu sina hamu! Alijizuga kunitukuza wakati ukweli alijitukuza na kujikweza. Alijifanya rafiki na kipenzi changu kumbe adui mkubwa nyambaff!

Juzi nilimsikia akiwataka mafyatu wamuombee awe msemaji wa wanyonge. Je, mimi siyo msemaji wao au nawatesa? Hiki kifyatu kinachofyatuka nilipokiteua, nilidhani kingenifaa. Kumbe kilitaka kunitumia kujitengenezea ulaji japo mafyatu sijui kama ni mazwazwa wakipewa hata ujumbe wa nyumba kumi.

Juzi, mkwe wangu alipigiwa simu na kidhabu huyu na kunilalamikia. Ndugu yangu mwingine alihoji ilikuwaje nikateua kituko hiki kinachoniaibisha na chata langu!

Aliuliza kwa uchungu kama ni washauri walionishauri, niwafyatue kabla huyu kidhabi hajanifyatua kwa kufanya mafyatu wanifyatue kwenye uchakachuaji ujao.

Wasaidizi wangu wengi walilalamika kuwa fyatu huyu kihiyo alikuwa akiwaingilia kwenye nafasi zao asijue kazi yangu kubwa ni kuteua na kutengua kwa mujibu wa katiba yetu fyatu ya mafyatu.

Badala ya kufuata kanuni za uongozi, alizivunja zote. Kugundua aliniona zwazwa akizidisha kabobo, nilimtengulia mbali. Kumbe mtangulizi wangu aliyemtupa jalalani alikomtoa hakukosea.

Nimeaibika, kuhuzunika, kushangaa, na kujifunza sana. Sijui ni kukata tamaa au uzembe, maana hata mafyatu wanamuamini wasijue janja ya nyani na wanaingizwa chaka na mkenge mchana kweupe! Je, kuna kitu hatukuelewa uzuri au tulipitiwa? Inakuwaje fyatu, tena asiye na chochote, kujifanya anaweza kutatua matatizo yote wakati hana uwezo?

Kwa kutumia jina langu, alijijengea imani, umaarufu, na sifa asizo nazo. Kwa makusudi, alijua hatatui bali kukuza matatizo ili baadaye ayatumie kutufyatua sisi tuliomfyatua na kumpa nafasi ambayo alitaka kuitumia kutufyatua. Ametufanya tuonekana wote kichekesho naye bonge la mjanja.

Alianza kuwachonganisha watendaji wangu katika kila idara akiwapigia simu hovyohovyo wengi ambao kimadaraka, wako juu yake kwa kusingizia chata letu. Juzi hata mshirika wangu kanishauri niachane na kijitapeli hiki kichumiatumbo kinachoota kuna siku kitakuwa M/kiti na rahisi wa mafyatu.

Kwa ujuha, kidhabi huyu alidhani nilimteua kama kijibwa cha kuwatisha wanene. Siri kali haiendeshwi hivyo. Ni M/kiti mshamba anayeweza kutengeneza vijimbwa na vichawa kuwatisha wasaidizi wake.

Kama unajiamini kama mimi unateua na kutengulia mbali bila kuangalia sura ya nyani. Si una dola. Siku hizi ni rahisi kwa rahisi kuteua na kutengua. Kumejaa machawa na mafyatu wanaojipendekeza wakijiruhusu kubadilishwa kama nepi mradi wapate tonge.

Du! Hamjanielewa walengwa?