Kwa sheria zetu ukahaba si biashara halali

Biashara ya ukahaba yashamiri-2

Mabadiliko ya teknolojia yaliyopo hivi sasa duniani yamerahisisha mawasiliano na kusaidia huduma mbalimbali kuwa bora na hivyo kuongeza ufanisi kwa mtu mmoja mmoja, Taifa na dunia.

Matumizi ya vifaa vya kisasa, zikiwemo simu, kompyuta, vishkwambi yamekuwa ni sehemu ya maisha ya kila siku kwa walimu na wanafunzi na hivyo nyezo za kufundishia na kujifunzia zimerahisishwa na kwenda mahitaji ya sasa.

Kutokana na umuhimu wa maendeleo hayo katika kila nyanja ya maisha, Tanzania, ikiwa sehemu ya ulimwengu wa teknolojia, nayo inapaswa kuweka nguvu zaidi kwenye eneo hilo kwa kuwa yana faida nyingi.

Miongoni mwa faida hizo ni pamoja na ukusanyaji wa mapato, kufuatilia utendaji kazi, kupanga na kutekeleza programu mbalimbali zenye tija kwa wananchi, matibabu, viwanda, vyombo vya usafiri na mawasiliano mengine kwa ujumla.

Katika muktadha huu ni imani yetu kuwa somo la kompyuta na mengine yanayohusiana na teknolojia ya kisasa yanapaswa kufundishwa kwa vitendo kuanzia shule za msingi hadi vyuoni.

Tumemsikia Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo, akishauri vyuo vya ufundi stadi nchini (Veta) vifundishe kompyuta kama somo la lazima ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia ili kumwezesha mwanafunzi kuwa na uelewa mpana utakaomsaidia kujiajiri au kuajiriwa.

Pamoja na hayo, tumeshtushwa kusikia somo la kompyuta halijawa la lazima hata vyuo kama Veta wakati katika mazingira ya sasa, hatupaswi kuzungumzia matumizi ya kompyuta kwenye vyuo, bali hilo tulisikia likishushwa katika shule za msingi na sekondari.

Tunaamini nchi haiwezi kupiga hatua kubwa za maendeleo kama matumizi ya teknolojia ya kisasa hayatakuwa ya kiwango kikubwa kwa wananchi

Tunajua baadhi ya shule za msingi, hasa za binafsi matumizi ya kompyuta hivi sasa ni jambo la kawaida tofauti na zile za Serikali ambapo ni chache zenye kufundisha somo la kompyuta.

Hatutaki somo la kompyuta lifundishwe pasi na wanafunzi kuiona na kuitumia, bali wafundishwe kwa vitendo ili kuwajengea taswira halisi na uelewa zaidi.

Tunajua mwanafunzi anapojifunza kwa vitendo huwa si rahisi kusahau na huwa balozi wa kuwafundisha wengine.

Hatuoni sababu ya somo la kompyuta kutofundishwa kuanzia ngazi za chini kwa kuwa mara kwa mara CCM huweka kwenye ilani yake matumizi ya Tehama.

Pamoja na hatua kubwa iliyopigwa hivi karibuni kwa Serikali kugawa vishkwambi kwa walimu, tulitarajia kila mwaka CCM ingeisukuma Serikali kuongeza nguvu kwa kugawa vifaa vya teknolojia katika taasisi za elimu ili kuijengea jamii mazingira ya kutambua kuwa bila matumizi ya teknolojia maisha huwa magumu zaidi.

Katika mazingira ya sasa mashine za ufundi zimeunganishwa na mifumo ya kompyuta na teknolojia za kisasa, hivyo ni muhimu somo hilo likafundishwa sambamba na masomo mengine ili kuwaandaa vijana kutumia zana za kisasa.

Wengi wetu ni mashuhuda wa teknolojia ilivyoleta mapinduzi makubwa kwenye sekta ya afya ambapo daktari anaweza kutoa maelekezo ya matibabu akiwa mbali na mgonjwa, tumeona vipimo vikifanyika eneo moja na kutumwa jingine kwa ushauri wa kitabibu au hata upasuaji kwa njia ya matundu.

Kwenye elimu nako ni hivyohivyo, mwalimu anaweza kufundisha akiwa mbali na wanafunzi kwa kutumia njia ya video, tunaamini kila sekta ikiwa na uwekezaji mkubwa kwenye matumizi ya teknolojia ya kisasa tutapiga hatua.

Fikra za kudhani elimu ya ufundi siyo kwa ajili ya wasiokwenda shule kabisa zinaondolewa kwa Serikali kuwekeza zaidi katika matumizi ya teknolojia ikiwemo kugawa vifaa vya kisasa vya kujifunzia na kufundishia.