Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Madhara ya unywaji pombe yadhibitiwe

Hakuna kiwango salama cha unywaji wa pombe chenye faida katika mwili wa binadamu.

Pombe mara zote inahusishwa moja kwa moja na magonjwa yasiyoambukiza, na hili halina ubishi kwa sababu wanasayansi wanabainisha juu ya athari zake.

Inahusishwa na magonjwa ya kisukari, figo, saratani na presha, huku Shirika la Afya Duniani (WHO) likibainisha kuwa watu milioni 3 hupoteza maisha kila mwaka duniani kutokana na madhara ya unywaji wa pombe kupita kiasi.

Wanasayansi hao wanasema pombe si hitaji la muhimu kwenye mwili wa binadamu, bali mwili huhitaji vyakula vyenye protini, madini na virutubisho vingine muhimu ili kuufanya ustawi na mtu anayekunywa pombe kupita kiasi, kuupa kazi ya ziada ya kubadili kemikali pombe ili iingie katika mahitaji ya mwili.

Chama cha Afya ya Jamii Tanzania kimekuwa kikitoa elimu kwa jamii kutambua kuwa pombe ina madhara na wachukue tahadhari katika matumizi yake.

Na moja ya hasara anayopata mnywaji wa pombe kupita kiasi ni kujishushia heshima mbele ya jamii na kudharaulika.

Nami nichukue nafasi japo kidogo ya kuungana na madaktari kukiri kuwa ni kweli pombe ina madhara.

Katika kukabiliana na athari zinazotokana na matumizi ya pombe, nchi ya Urusi imeweka marufuku kwa mtu kunywa pombe barabarani, mtaani na anayevunja marufuku hiyo hukamatwa na kutozwa faini na vyombo vya dola baada ya serikali ya nchi hiyo kubaini madhara yake.

Lakini kwa mujibu wa WHO, imeitaja nchi ya Urusi kuwa watu wake wamepunguza unywaji wa pombe kupita kiasi kwa asilimia 43 kutoka mwaka 2003 hadi 2016.

Inaelezwa hatua hiyo imekuja baada ya taifa hilo kuchukua hatua kadhaa za kuwasukuma watu kubadili mifumo yao ya maisha na kuishi kwa kuzingatia afya zao.

Dunia inatambua taifa la Urusi linaongoza kwa unywaji wa pombe kupita kiasi, kwa nini Tanzania isianze kuchukua hatua za makusudi kuwakanya wananchi wake kupunguza unywaji pombe uliopitiliza? Licha ya madhara yaliyobainishwa na wanasayasi na madaktari juu ya athari za kiafya inayotokana na unywaji pombe, lipo tatizo lingine la uwepo wa pombe feki, hali inayoongeza tatizo kubwa la kiafya kwa mnywaji kutokana na pombe hizo kutopita katika vipimo vinavyokubalika kimaabara.

Na tukumbuke kuwa wanaokunywa mara zote huwa hawaangalii madhara ya baadaye, hali inayosababisha mzigo kwa familia pindi mnywaji huyu anapokuwa ameathirika na pombe.

Wengi wao huugua figo, ini, moyo, sukari, shinikizo la damu na maradhi kadha wa kadha.

Hivyo mzigo wote wa kuwatibu familia hujikuta zikiubeba na hata Serikali pia.

Unywaji wa pombe umekithiri katika makundi mbalimbali na watoto chini ya miaka 18 hujiingiza katika ulevi.

Viwango vinaainisha kuwa mnywaji anapaswa anywe angalau wastani wa lita 9.1 kwa mtu mmoja ndani ya mwaka mmoja, lakini mtu ajipime mwenyewe kiwango hicho kinazingatiwa au hunywa zaidi ya lita 9.1 kwa mwaka.

Uongozi wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania umekuwa ukibeba jukumu zito la kutoa elimu juu ya madhara ya unywaji wa pombe, ikitoa elimu na uchunguzi.

Chama hicho kinafanya utafiti kwa mikoa minne ya Kilimanjaro (Hai), Morogoro (Kilosa), Manyara (Babati) na Dodoma mjini, unaolenga kuchunguza madhara, unywaji na kuja na mpango wa kutoa elimu juu ya madhara ya unywaji pombe ili jamii ichukue hatua.

Pamoja na pombe kuleta faida kwa pato la taifa, bado tafiti zinaonyesha ina madhara katika kipato cha taifa, kiafya, kijamii, kiuchumi na athari nyingine.

Serikali ya Mtaa hadi Wilaya imekuwa ikifumbia macho ukiukwaji na usimamizi wa sheria ya pombe inaposhindwa kudhibiti wamiliki wa baa kwa watu kuanza kunywa pombe kuanzia saa 1 asubuhi badala ya saa 9 alasiri.

Jambo hili linawafanya wanywaji wa pombe kuwa wengi, baadhi yao wakiwa watumishi wa Serikali, taasisi na mashirika ya umma na kurudi nyuma kwa mchango wa mtumishi husika katika maendeleo ya taifa.

Serikali pia itupie jicho kundi lingine linalochangia matatizo ya wananchi kupatwa na magonjwa yasiyoambukiza, hasa katika kamari za mashine maarufu kama Dubwi, ambazo zimetapakaa kila kona ya mitaa ya mijini na vijijini ambapo imekuwa chanzo kizuri cha vijana kupata mitaji ya fedha na kununua pombe.

Mashine za kucheza kamari zimempa urahisi kijana kupata fedha za kununua pombe, dawa za kulevya za aina mbalimbali, hivyo ni maeneo hatari kwa watoto kutokana na uwepo wake maeneo ya mitaa na maeneo husika mmomonyoko wa maadili ni mkubwa.