Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwaka wa kufosi umeisha, sasa mjipange

Mwaka huu ulianza na msemo maarufu kwamba ndio mwaka wa kufosi, yaani ni mwaka wa kupambana mpaka kieleweke, kufanya kazi kwa bidii kufa kupona na kufikia malengo. Yaani hakuna kulala hadi kieleweke.

Msemo huu ulikuwa maarufu sana na sasa tumefika mwishoni mwa mwaka 2024, tunageuka nyuma na kuanza kuangalia tumefanya nini. Tunapomalizia siku hizi tano hebu tufanye tathimini ya kina. Tuhesabu faida na hasara halafu tupange upya.

Wako watu walianza kwa kasi hawakufikia mwisho, hajavuna, walikuwa na nguvu ya soda, wako waliokomaa wakafosi mpaka jana wakapata matokeo kidogo na wako waliopata kama walivyopanga.

Nimeona wengine wakitimiza malengo kiulaini, bila kutoka jasho sana, huku wengine wakitoa jasho la damu, lakini wakapata haba. Hayo ndiyo maisha yanahitaji mpango na mkakati makini hasa.

Nimeona wengine wakivunjiwa mkataba (Gamond et al), nimeona wengine wakipewa mkataba mpya wenye vifungu vyenye posho nene, wengine wakishinda uchaguzi huku wakifanikiwa kuanzisha biashara mpya.

Wengine wameanza masomo na wengine wamehitimu masomo baada ya kusup mara kadhaa. Wengine wameongeza familia kwa kuoa na kuolewa au kuongeza mtoto. Jambo muhimu kujua katika mambo yote uliyojipangia umepiga hatua gani? Jilinganishe wewe binafsi na sio na jirani au rafiki, haina afya hiyo. Jipime na mwaka jana wako.

Nakubali kuanza mwaka bila kitu sio kosa lako, lakini kumaliza bila matokeo chanya ni kosa lako na unawajibika kwa yote.

Nafahamu wako ambao hawajafosi chochote sio kwa sababu hawana kitu, bali ni kwa kuahirisha mambo (procastinate) kila wanapotaka kuanza, yaani ingia toka nyingi, nitaanza kesho za kutosha hamadi Desemba 27 hii hapa. Tunapoangalia tunauliza kiko wapi, tumetoka wapi, nini tumepata mwaka mzima, tunaona maneno tu.

Tukihesabu baraka tunaziona, ukiangalia tumezitumiaje wote tunabaki mdomo wazi na waliojasiri wanasema nimetoka kapa.

Tumia kanuni ya 80/20, maarufu kama kanuni ya Pareto (Pareto principle) iliyoasisiwa na mchumi mashuhuri wa Kiitaliano Vilfredo Pareto. Ni kwamba matokeo uliyoyapata yanatokana na juhudi zako.

Pareto anasema asilimia 80 ya matokeo unayoyapata yanatokana na asilimia 20 ya juhudi zako. Sasa tathmini kama umepata mafanikio kidogo basi uliwekeza jitihada chini ya asilimia 20 (hatari sana). Kwa maneno mengine, wewe mwenyewe umejikatili kufikia malengo yako kwa kuwekeza jitihada kidogo.

Hebu piga picha (imagine) tungeweza kuwekeza zaidi jitihada zetu pengine zaidi ya asilimia 20 kidogo tu ingekuwaje. Tungepata matokeo makubwa isivyo kawaida, yes beyond obvious.

Sasa, ya kale hayanuki, ngoja tugange yajayo. Yaani sasa tujitahidi kuongeza jitihada zetu walau tufikie asilimia 20 tutapata A plus ya asilimia 80.

Mwaka wa kufosi ulioanza kwa kuvimba macho unafikia mwisho, ndiyo tumalize vizuri hizi siku chache kwa kupanga upya namna tutakavyoweka asilimia 20.

Tuwekeze ubunifu wetu kwa asilimia 20 tutatoboa, tupate wateja asilimia 20 tutapata faida asilimia 80, ukifanya hivi ushindi ni hakika.

Naomba nihitimishe kwa msemo huu "I never lose. I either win or learn. - Nelson Mandela”, ndiyo, kama hukutimiza malengo basi kweli hukushindwa, bali ulijifunza kuwa unaweza kufanya vizuri zaidi, basi chukua hatua na kutekeleza malengo yako.

Safari hii jaribu tena kupanga, jaribu tena, ongeza bidii, punguza orodha ya mambo, panga na tekeleza kwa kuzingatia vipaumbele.

Yako mambo mawili uyazingatie sana, nayo ni ongeza maarifa na tunza afya yako, maarifa yatakuwezesha kukabili yaliyoko mbele pale tu utakapokuwa na afya njema.

Ongeza maarifa kwa kusoma kitabu angalau kimoja, tembea usikae sehemu moja mwaka mzima, jifunze mambo mapya, angalia movie zenye mafunzo, fanya kozi fupi fupi na kadhalika.

Tunza afya yako kwa kula vizuri, kufanya mazoezi, kufuata maelekezo, kuzingatia kunywa dawa kwa wakati, kupumzika na kulala vizuri. Kama 2024 ulikuwa wa kufosi, huu unaokuja tunaupa jina gani?

Nakutakia heri na fanaka ya sikukuu za Noeli na Mwaka mpya mwema. It is better to aim high and miss than to aim low and hit (muulize jirani yako Kiswahili cha msemo huu).