Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msanii ni yule anaye burudisha, kuelimisha

Kalunde Jamal

Muktasari:

Huu ni utamaduni wao na kizuri zaidi ugomvi wao ndiyo unaowafanya wazidi kufanya vizuri kwenye shoo zao mbali mbali.Kwa maana ya kuwafanya wawe mastaa na wajulikane sehemu mbali mbali ikiwamo Afrika.

Wanamuziki wa Marekani, Chris Brown na Drake walishambuliana katika klabu moja na ilidaiwa chanzo cha ugomvi wao ni kumgombania mwanamuziki mwenzao Rihanna, habari hii niliisoma Juni 14 mwaka jana, lakini wasanii hao wote wana hela na kila mmoja ana biashara zake nje ya muziki zinazomuingizia kipato.

Huu ni utamaduni wao na kizuri zaidi ugomvi wao ndiyo unaowafanya wazidi kufanya vizuri kwenye shoo zao mbali mbali.Kwa maana ya kuwafanya wawe mastaa na wajulikane sehemu mbali mbali ikiwamo Afrika.

Lakini Nick Minaj, Mariah Carey, wanagombana mara nyingi kwenye mashindano ya American Pop Idol, hao wote ni wasanii wakubwa na wenye uwezo wa kufanya kazi hasa za burudani na kugombana kwao ni katika kutafuta hela na si vinginevyo.

Wasanii wote hao niliokutajia, pesa wanayoipata wakipiga shoo moja, wasanii wa hapa nyumbani watapiga miaka mitatu kuipata. Hapo unaweza kuona tofauti kubwa iliyopo.

Kuna wasanii wa Kimarekani ambao wamekuwa kila kukicha wanakumbwa na kashfa za kupigana na vitu kama hivyo lakini ukifungua ‘profaili’ zao ni watu wakubwa wana miradi mingi wana hela nyingi na wanaweza kuishi bila muziki, lakini kizuri zaidi ndio utamaduni wao kufanya hivyo.

Upepo wa wasanii kushambuliana umeingia kwetu, hivi karibuni wasanii kadhaa wamerushiana ngumi, makopo, chupa n.k. Hivi kuiga vitu kama hivi kunawafaidisha vipi wasanii wetu?

Kinachonisikitisha ni kwamba wasanii hao wanaopigana hata shoo zao zinahesabika kwa mwaka, wanatoa albamu bila kuwa na shoo, hakuna kitu ambacho wamefanya kwenye tasnia hii ya muziki kikaishtua jamii.

Sijaona kitu hata kimoja kinachowafanya wapigane wala kugombana huku enzi zao za muziki zimekwisha na kama zipo siyo kivile.

Nanukuu maneno ya msanii nguli katika tasnia hii ambaye nafikiri ni miongoni mwa wasanii walioipa chati tasnia hii ya muziki wa Bongofleva, Profesa Jay.”

Ilituchukua muda sana kuhakikisha tunaufikisha muziki huu hapa ulipo, jamii imeuchukulia sasa imetukubali” mwisho wa kumnukuu.

Hapa unaweza kuona ni kwa jinsi gani wasanii wakongwe walivyopata taabu kuufanya muziki huu, lakini wasanii wachache ambao nafikiri wamechoka kuitwa wasanii wanataka kuitwa mabondia, wanaamua kuuvunjia heshima kwa kupigana ovyo hadharani bila kujali kama kufanya hivyo ni kosa la jinai.

Ushauri wangu kwao nikiwa kama mdau wa burudani, kama wamepata njia nyingine ya kutafuta fedha tofauti na muziki wawaache wasanii wenye mapenzi mema na tasnia hii muhimu iliyotoa ajira kwa vijana wengi.

Wasiharibu kile wenzao walichokitafuta na kukifanya kwa muda mrefu kwa sababu ya kuishiwa au kutafuta sifa zisizo na msingi.

Hayo mambo ya kupigana watu waliyaacha tangu miaka mingi iliyopita lakini wao kwa kuwa hawajitambui bado wanayafanya, tumechoka kuwasikia.
Kwa tabia yao hiyo tunashindwa hata kwenda kwenye shoo ambazo pengine zisingekuwa na fujo.

Wamekuwa wakichukua muda mwingi kuhakikisha zinatokea vurugu, ambazo zinasababisha kuvuruga amani, kuharibu akili ya wapenda burudani na kuifanya jamii ikidharau kile ambacho kimeshakuwa na kutoa matunda.

Msanii ni yule anayeburudisha na kuelimisha na siyo anayegombana au kupigana, hivi ni vitu ambavyo havielemishi wala kuburudisha.

Mnajiita kioo cha jamii wakati hamana mng’aro zaidi ya kuwapa mashabiki wenu ‘sintofahamu’ na kushindwa kuelewa nia yenu hasa ni nini katika tasnia hii iliyojipatia umaarufu mkubwa kutokana na kuokoa vijana walio wengi,kwa kuwapatia ajira.

Sidhani kama kuna anayependa kukiona hiki mnachokifanya iwe wasanii wenzenu, wapenda burudani na wadhamini wa burudani kwa jumla.

Ninachoweza kuwaambia nyie wote msiojitambua kwenye hii tasnia hii, achieni ngazi labda mmeshindwa kufanya muziki na mnataka kufanya kitu kingine.
Heshimuni mashabiki wenu kwani kupigana mbele yao ni kuwashushia heshima.

Pia kumbukeni kuwa wapo waliojitoa kuufanya muziki huu ufike hapa, hivyo ni jukumu lenu sasa kuupeleka katika ngazi za juu.

Kutumia ugomvi kama njia ya kujitangaza pia hiyo ni dalili kuwa huwa kipaji. Ukiona umefikia hatua hiyo taratibu anza kutafuta kitu kingine cha kufanya.

Kwa pamoja tusaidiane kuipeleka Bongo Fleva katika anga za kimataifa. Mungu ubariki muziki wetu, Mungu ibariki Tanzania.

0755695104