Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa Afrika waliotikisa Ligi ya Mabingwa Ulaya

Ndoto ya Mbwana Samatta kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imetimia, baada ya kusota muda mrefu akiishuhudia timu yake ya Manchester United katika runinga.

Nahodha huyo wa Taifa Stars ni shabiki wa Man United na hafichi hisia zake kwa aliyekuwa kocha wa timu hiyo Sir Alex Ferguson.

Samatta alitamani siku moja kucheza ligi hiyo yenye mvuto na ushindani wa aina yake. Kiu yake ilikuwa kufikia mafanikio ya aliyekuwa kinara wa mabao Arsenal Thierry Henry.

Mshambuliaji huyo anasema pamoja na kuipenda Man United, lakini nahodha huyo wa zamani wa Arsenal na Ufaransa alikuwa akimuhusudu.

Ndoto ya Samatta imetimia. Sasa ni mchezaji wa kimataifa mwenye kiwango cha juu anayewindwa na klabu za Ulaya baada ya kutamba KRC Genk ya Ubelgiji.

Newcastle United, Everton, West Ham United na Burnley za Ligi Kuu England zimeingia vitani kuwania saini ya Samatta.

Baada ya kucheza African Lyon kati ya mwaka 2008 na 2009, Simba ilimnasa ambapo alicheza kwa muda mfupi tu kabla ya kupigwa bei TP Mazembe ya DR Congo alikocheza kwa mafanikio kabla ya kutua Genk.

Ndoto ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya ilitimia Septemba 17 baada ya kucheza mchezo wa kwanza dhidi ya Salzburg, licha ya timu yake kufungwa mabao 6-2. Samatta alifunga bao moja.

“Nilikuwa nikiangalia Ligi ya Mabingwa na England ni michuano mikubwa kila kijana wa nyumbani (Tanzania) anapenda kuangalia. Mimi nilitamani kucheza,” anasema.

Samatta amefunga mabao mawili katika michuano hiyo likiwemo dhidi ya Liverpool katika mchezo anaosema utabaki kichwani mwake licha ya kufungwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Anfield.

Samatta anakuwa mchezaji wa pili kutoka Afrika Mashariki nyuma ya Victor Wanyama wa Tottenham Hotspurs kucheza kwenye uwanja huo wenye mashabiki watukutu.

Spoti Mikiki linakuletea orodha ya wachezaji wa Afrika waliong’ara wiki iliyopita katika michezo ya raundi ya nne ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika hatua ya makundi.

Mbwana Samatta vs Liverpool

Samatta (26) ambaye anakuwa mchezaji wa kwanza wa Afrika Mashariki kucheza na kufunga bao katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya alipofunga dhidi ya Liverpool.

Katika mchezo huo, Samatta amewazidi kete Waafrika wenzake walioambulia patupu, Mohammed Salah aliyecheza kwa dakika zote tisini ambaye ni raia wa Misri na Msenegal Sadio Mane aliyeingia dakika ya 75 kuchukua nafasi ya Oxlade Chamberlain.

Bertrand Traore vs Benfica

Traore ni mshambuliaji wa Burkinafaso anayecheza Lyon alikuwa kati ya wafungaji wa klabu hiyo ya Ligi Kuu Ufaransa ambao walifunga katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya wapinzani wao wa Ureno.

Katika mchezo huo, Lyon iliibuka na ushindi wa mabao 3-1, bao la kwanza lilifungwa na Joachim Andersen la pili likifungwa na Memphis Depay huku la tatu akifunga Traore ambaye aliwahi kucheza Chelsea.

Geoffrey Kondogbia vs Lille

Mchezaji wa kimataifa wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Kondogbia akiwa na Valencia ya Hispania, alifunga bao timu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Lille ya Ligi Kuu Ufaransa.

Mchezaji huyo wa zamani wa Inter Milan na Monaco, alifunga bao hilo, dakika ya 84, akimalizia pasi ya Maximiliano Gomez. Mabao mengine ya Valencia yalifungwa na Daniel Parejo na Ferran Torres huku jingine wakijifunga kupitia kwa Adama Soumaoro.

Victor Osimhen vs Valencia

Mchezaji wa Nigeria ambaye anacheza Lille ya Ufaransa, Osimhen licha ya timu yake kopoteza katika raundi ya nne ndiye aliyefunga bao la kufutia machozi katika kipigo walichopata cha mabao 4-1 kwenye Uwanja wa Mestalla, Hispania.

Aina ya uchezaji wa Osimhen mwenye miaka 20 inafananishwa na Tammy Abraham wa Chelsea ambaye asili yake ni Nigeria pamoja na kuchagua kwake kuitumikia timu ya taifa ya England ambako amekulia.

Achraf Hakimi vs Inter Milan

Mmorocco anayecheza kwa mkopo Borussia Dortmund akitokea Real Madrid, aliibeba klabu hiyo ya Ujeruma kwa kufunga mabao mawili, yaliyochangia ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Inter Milan inayonolewa na Antonio Conte.

Inter Milan ikiwa na mshambuliaji wao Romelu Lukaku iliitangulia Dortmund kwa mabao mawili kabla ya Hakimi kufunga bao la kwanza kwa timu hiyo huku Julian Brandt akifunga la kusawazisha kabla ya Mmorocco huyo kufunga la ushindi.

Hakim Ziyech vs Chelsea

Hakumaliza dakika zote tisini katika mchezo dhidi ya Chelsea baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu wachezaji wawili Daley Blind aliyewahi kucheza Manchester United na Joel Veltman, ilibidi atolewe na kocha wa Ajax, Erik ten Hag.

Hag alibadili mbinu kwa kuingiza mabeki hata hivyo Ziyech, aliifunga Chelsea bao la tatu kwa mpira wa faulo ambao ulimgonga Kepa Arrizabalaga hakuishia hapo. Winga huyo msumbufu alitengeneza bao la pili la Ajax, lililofungwa na Quincy Promes na nne, alilofunga Donny van de Beek.

Kama si kupungua Ajax , pengine ingekuwa inazungumzwa habari nyingine kuhusu mchezo huo, ambao baada ya kuonyeshwa kadi za mbili za njano wachezaji hao, Chelsea ilifunga mabao mawili ya haraka ndani ya dakika nne kupitia kwa Jorginho na Reece James.