Soka la Tanzania mashakani

Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Dk Fenella Mukangara akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mgogoro wa uchaguzi wa viongozi wa Shirikisho la Soka tTanzania (TFF) Picha na Michael Matemanga
Muktasari:
Sheria za Fifa zinazuia Serikali kuingilia kwa namna yoyote kwenye suala la utawala wa soka nchini. Kama Serikali ikikaidi suala hilo nchi husika inafungiwa kushiriki mashindano yote ikiwamo Kombe la Afrika, Dunia pamoja na kufutiwa misaada yote wanayopewa na Fifa.
TANZANIA huenda ikajikuta matatani na Shirikisho la Soka Kimataifa (FIifaFA) baada ya Serikali kuingilia kuifuta katiba mpya ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Sheria za Fifa zinazuia Serikali kuingilia kwa namna yoyote kwenye suala la utawala wa soka nchini. Kama Serikali ikikaidi suala hilo nchi husika inafungiwa kushiriki mashindano yote ikiwamo Kombe la Afrika, Dunia pamoja na kufutiwa misaada yote wanayopewa na Fifa.
Hali hiyo itaweka matatani ushiriki wa timu za Simba na Azam kwenye mashindano ya klabu barani Afrika. Pia Taifa Stars inayoshiriki kwenye michuano ya awali ya Kombe la Dunia.
Mapema jana, Waziri wa Habari Utamaduni Vijana na Michezo, Dk Fennela Mukangara alisema Baraza la Michezo Tanzania (BMT) haliitambui katiba iliyotumika katika mchakato wa uchaguzi mkuu wa TFF na badala yake wanatambua katiba ya mwaka 2006.
Mwaka jana TFF ilipitisha waraka kwa wajumbe wake kwa ajili ya mabadiliko ya katiba ili kutimiza matakwa ya Fifa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), ambapo asilimia 70 ya wajumbe walikubali mapendekezo ya waraka huo ambao ulileta katiba mpya ya TFF ya 2012.
Kauli ya Mukangara imekuja baada ya kutokea mkanganyiko mkubwa katika uchaguzi huo ambao tayari Fifa imeusimamisha hadi pale wajumbe wake watapokuja nchini kuangalia umapungufu wyake kabla ya kutoa hatima ya kufanyika kwake.
Waziri Dk Mukangara alisema wao kama Serikali hawatambui katiba iliyotumika katika kutoa uamuzi na badala yake wameitaka TFF kufuta matumizi ya katiba ya mwaka jana kwani imekiuka kanuni za sheria ya BMT, namba11, ibara ya 1.
“Natoa agizo kwa wasaidizi wa msajili wa vyama kote nchini kufuata taratibu za usajili kwa mujibu wa sheria na kanuni za BMT, sisi hatuitambui katiba iliyotumika katika mchakato wa uchaguzi wa mwaka huu na sasa badala yake tunatambua ile ya mwaka 2006, hii ni batili na imekiukia kanuni na sheria za BMT,”alisema Dk Mukangara.
Alisema kuwa Msajili wa Vvyama vya Mmichezo wa Taifa, Mercy Rwezahura aliyedaiwa kuipitisha katiba hiyo ameondolewa na tayari mchakato wa kumtafuta mwingine umeanza.
Alisema licha ya kupata taarifa za ujio wa wajumbe kutoka Fifa ametoa agizo kwa TFF kuwataarifu Fifa kuhusu maelekezo hayo ya kutumia katiba ya mwaka 2006 na kuwaeleza hali halisi.
“Naelekeza na ifahamike kuwa hakuna chama chochote cha michezo kilicho juu ya BMT na naelekeza, pia TFF waitishe mkutano mkuu kwa misingi ya kKatiba yao ya mwaka 2006 na kama kuna umuhimu wa kubadilisha ifanye hivyo mara moja,”alisema Dk Mukangara.
Mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa TFF ulisimamishwa kutokana na mgogoro mzito uliotokana na kuenguliwa kiutata kwa wagombea kadhaa, wakiwamo Jamal Malinzi anayewania urais na Michael Wambura anayetaka kugombea nafasi ya makamu wa rais na .
Kamati ya Rufaa ya TFF inayoongozwa na Iddi Mtiginjola ndiyo ilisimamia zoezi zima la kuwaengua kina Malinzi na kumuacha Makamu wa sasa wa Rais, Athumani Nyamlani abaki kuwa mgombea pekee.
Mwananchi ilimtafuta Katibu mkuu wa TFF, Angetile Osiah kutaka kujua msimamo wao alisema kwanza kabisa wanashangazwa na kauli ya wWaziri kwani kila wanapofanya mabadiliko ni lazima ajenda za mabadiliko zitambulike kwa wWizara husika.
“Akisema anatambua katiba ya mwaka 2006, ina maana hatambui mabadiliko mengine yoyote, kama hatambui basi hata Ligi Kuu haitambuliki, mashindano ya kimataifa yanayozishirikisha Simba na Azam pia hayatambuliki kwani katiba iliyotumika ni ya mwaka 2012,”alisema Osiah.
Alisema kuwa tayari wamepeleka katiba yao ya 2012 Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na ndiyo inayotumika kwa sasa hata katika ujio wa ujumbe wa Fifa na kusisitiza kauli ya wWaziri haikusimama katika ukweli na itazidi kupotosha umma wa mashabiki wa soka.
“Tumekuwa tukifanya mabadiliko mengi tangu 2006 hadi mwaka jana ina maana hayo mabadiliko yote hayatambui?, Mikoa ya Katavi, Geita, Simiyu inatambulika kwa sasa kama mikoa wanachama wapya kupitia mabadiliko ya Katiba hiyo nayo ifutwe kwa sababu tu katiba iliyotumika si sahihi, kiukweli kauli yake imetushangaza sana,”alisema Osiah.
Ikiwa Tanzania itaadhibiwa Fifa tena safari hii itakuwa mara ya tatu kwani imewahi kusimamishwa mara mbili.
Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1996 baada ya BMT kuchuja baadhi ya wagombea kuwania uchaguzi wa FAT na mwaka 2001 kufuatia kitendo cha Serikali kuvunja uongozi wa FAT na kuteua Kamati ya Muda.