Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Afrika ya Kati yaaga CHAN, Madagascar yafufua matumaini

Muktasari:

  • Fainali za CHAN 2024 ni za kwanza kwa timu ya taifa ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kushiriki ikitokea kanda ya soka ya UNIFFAC.

Jamhuri ya Afrika ya Kati leo Agosti 13, 2025 imekuwa timu ya pili kuaga Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) 2024 ikifuata nyayo za Nigeria.

Kichapo cha mabao 2-0 ilichokipata kutoka kwa Madagascar kimeifanya Afrika ya Kati kubaki mkiani mwa kundi B la mashindano hayo ikiwa haina pointi, matokeo yanayoifanya iage rasmi kwani hata ikipata ushindi katika mechi ya mwisho dhidi ya Tanzania ‘Taifa Stars haitoweza kumaliza katika nafasi mbili za juu kwenye kundi hilo.

Bao la kwanza la Madagascar katika mchezo huo wa leo dhisi ya Afrika ya Kati limepachikwa na Toky Rakotondraibe katika dakika ya 84.

Wakati Jamhuri ya Afrika ya Kati wakijipapatua kusawazisha, Lalaina
Rafanomezantsoa aliipatia Madagascar bao la pili katika dakika za majeruhi ambalo lilizika rasmi matumaini ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kubaki katika mashindano hayo.

Umekuwa ni ushiriki usio mzuri kwa Jamhuri ya Afrika ya Kati inayoshiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza kwani ndio imekuwa kibonde wa kundi hilo.

Kabla ya kichapo cha leo, ilianza kufungwa mabao 4-2 na Burkina Faso kisha ikafungwa bao 1-0 na Mauritania.

Kwa ushindi wa leo, Madagascar sasa imeweka hai matumaini yake ya kufuzu robo fainali kupitia kundi hilo kwani imefikisha pointi nne.

Madagascar inaungana na timu za Burkina Faso na Mauritania kuwania nafasi moja iliyobakia katika kundi hilo kwa vile tayari nyingine moja imeshanyakuliwa na Taifa Stars