Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aguerd awapasua kichwa Morocco

Beki wa kati wa timu ya Taifa ya Morocco, Nayef Aguerd ambaye bado anasumbuliwa na misuli ya nyonga. Picha na Maktaba

Kocha mkuu wa Morocco, Mohamed Ouahbi, amesema bado haijulikani kama beki wa kati chaguo la kwanza, Nayef Aguerd, atakuwa tayari kushiriki Kombe la Dunia , na kwamba wanaweza kumchukua mbadala wake iwapo hali yake haitaimarika.

Aguerd anayechezea Olympique Marseille, hajaonekana uwanjani tangu Machi 4 mwaka huu kutokana na matatizo ya muda mrefu ya misuli ya nyonga. Majeraha hayo yalipelekewa afanyiwe upasuaji mwezi Machi.

Kocha Ouahbi ambaye amemjumuisha Aguerd kikosini licha ya mchezaji huyo kutokuwa fiti, amesema kuwa bado wana matumaini naye na ikishindikana kutumika, wameandaa mtu wa kuziba nafasi yake.

Beki wa kati wa timu ya Taifa ya Morocco, Nayef Aguerd ambaye bado anasumbuliwa na misuli ya nyonga. Picha na Maktaba

“Bado tuna muda wa kufanya uamuzi na tutaendelea kufuata utaratibu wa kitabibu, lakini pia tunaye Marwane Saadane ambaye yupo hapa," alisema Ouahbi.

Beki wa Al-Fateh, Marwane Saadane, kwa sasa yupo kambini na timu licha ya kutokuwamo kwenye kikosi rasmi cha wachezaji 26.

Ouahbi amethibitisha kuwa ameendelea kubaki kambini kama mbadala wa Aguerd iwapo beki huyo wa zamani wa West Ham United hatapona kwa wakati.

Beki wa kati wa timu ya Taifa ya Morocco, Nayef Aguerd ambaye bado anasumbuliwa na misuli ya nyonga. Picha na Maktaba

Mbali na Aguerd, Ouahbi anaweza pia kuwategemea mabeki wa kati Issa Diop, Chadi Riad na Redouane Halhal, ingawa wote wanakosa uzoefu mkubwa wa kimataifa.

Wachezaji waliokuwa washirika wake wa Aguerd katika safu ya ulinzi, Romain Saïss na Jawad El Yamiq, hawakuitwa na Ouahbi.