Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

APR, KMC zaanza vizuri Kombe la Kagame

Muktasari:

  • APR imechukua ubingwa wa Kombe la Kagame mara tatu ambazo ni 2004, 2007 na 2010.

Baada ya Singida Black Stars kulazimishwa sare tasa na Coffee ya Ethiopia jana, wawakilishi wengine wa Tanzania Bara katika Kombe la Kagame, KMC wameanza vyema mashindano hayo kwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mlandege ya Zanzibar.

Ikicheza mchezo wa kwanza wa kimashindano ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Marcio Maximo, KMC ililazimika kufanya kazi ya ziada kupata ushindi huo kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara ambayo ilipelekewa katika dakika za mwisho na Mlandege iliyokuwa inapambana kutafuta bao la kusawazisha.

Mabao ya ushindi ya KMC katika mchezo wa leo uliochezwa kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam yalipachikwa na Juma Shemvuni, Rashid Chambo na

Kwa upande wa Mlandege, mabao yake mawili katika mchezo huo wa kundi B yalipachikwa na Abeid Amaa na Aimar Haaland.

Kabla ya mchezo huo, ilishuhudiwa Mabingwa wa zamani wa mashindano hayo APR nao wakianza vyema kwa kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Bumamuru ya Burundi.

Ushindi huo wa APR leo ulitokana na mabao ya William Togui na Djibril Ouattara na kuifanya timu hiyo kukaa kileleni mwa msimamo wa kundi B ikifuatiwa na KMC.

Mara baada ya dakika 90 kumalizika, nyota wa APR Dao Meme alitangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mchezo.

Katika mchezo baina ya KMC na Mlandege, aliyeibuka mshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mchezo ni Redemtus Musa ambaye aliondoka na kitita cha Sh500,000.