Barbara ampongeza Nabi

Monday June 27 2022
ampongezapicc
By Ramadhan Elias

WAKATI Yanga ikiendelea kusherekea Ubingwa wake wa Ligi Kuu NBC kwa mara ya 28, Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amempongeza kocha Mkuu wa Wanajangwani hao Nassredine Nabi kwa kutwaa taji hilo.

Barbara kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika ujumbe uliosomeka  "Congratulations Coach" yenye maana ya hongera kocha huku akiambatanisha na picha mbili za Nabi.

Mwanaspoti linajua kuwa kabla ya Nabi kutua Yanga katikati ya msimu uliopita, kocha huyo alihusishwa kujiunga na Simba lakini dili hilo lilikwama na kutua Yanga.

Simba kwa sasa ipo kwenye mchakato wa kusaka kocha mpya baada ya kuachana na Mhispanyora Pablo Franco aliyeshindwa kufikia malengo ya timu na sasa kikosi kipo chini ya Seleman Matola aliyekuwa kocha msaidizi wa Pablo.

Advertisement