Bellamy azipa ubingwa Liverpool, Man City

Muktasari:
- Bellamy mzaliwa wa Wales amesema hazipi nafasi yoyote City, Tottenhma na Manchester United kung’aa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kama ilivyo kwa Liverpool ambayo tangu imeanza kunolewa na Jurgen Klopp imebadilika na sasa timu hiyo ndiyo bora kuliko kikosi chochote cha timu hiyo kwa misimu kumi iliyopita.
Kondon, England. Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Newcastle United na Manchester City, amesema anaamini Liver ina nafasi kubwa ya kufanya vema kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, kuliko timu nyingine za England.
Bellamy alisema mbali ya kuamini itafanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya lakini pia anaamini Liverpool itachuana na City mwanzo hadi mwisho katika mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England.
“Kwa upande wangu timu ya Liverpool ninaipa nafasi kubwa ya kufanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, kutokana na ubora wa kikosi chao, nadhani ndiyo mwakailishi imara wa England katika michuano hiyo tofauti na City, Man United na Spurs,” alisema.
Alisema katika Ligi Kuu England, mbali ya Liverpool timu nyingine ambayo itakuwa mshindani wa City kwenye mbio za ubingwa ni Chelsea ambayo msimu huu inaonekana kucheza soka la aina yake huku ikipata matokeo mazuri.
Alisema kuitendo cha Liverpool kushinda mechi tatu kati ya nne za mwisho kukutana na City kinathibitisha kuwa Klopp, anayo nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa England au kuitibulia timu kutetea ubingwa huo.
Aliupongez uamuzi wa klabu hiyo ya Merseyside kuwasajili Alisson Becker, Naby Keita, Fabinho na Xherdan Shaqiri katika dirisha la usajili wa mwaka kiangazi mwaka huu akisema umeimaarisha zaidi.
Liverpool kesho kutwa itaialika Napoli ya Italia katika mechi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya kushinda mechi ya kwanza kwa mabao 3-2 dhidi ya PSG ya Ufaransa.