Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Carrick alia na refa kipigo cha Leeds United

Muktasari:

  • Kichapo kutoka kwa Leeds United ni cha kwanza kwa Man United tangu 1981 na kimeifanya ibakie na pointi zake 55.

Manchester, England. Kaimu Meneja wa Manchester United, Michael Carrick ameshambulia uamuzi wa marefa kuwa ndio chanzo cha kupoteza kwa mabao 2-1 mchezo wa jana Jumatatu, Aprili 15, 2025 nyumbani dhidi ya Leeds United.

Kichapo kutoka kwa Leeds United ni cha kwanza kwa Man United kufungwa na timu hiyo tangu 1981 na kimeifanya ibakie na pointi zake 55.

Carrick amekasirishwa na kitendo cha Refa wa VAR, John Brooks kumshauri Refa wa Kati, Paul Tierney kwenda kutazama marejeo ya tukio la Lisandro Martinez kumvuta nywele Dominic Calvert-Lewin.

Baada ya Tierney kufanya marejeo ya tukio hilo, Martinez alionyeshwa kadi nyekundu na sasa anatarajiwa kukosa mechi tatu za timu hiyo.

Carrick anaamini kwamba uamuzi uliofanyika kwa Martinez haukuwa sahihi na ulichangia kuiathiri timu yake.

Beki wa kati wa Man United, Lisandro Martinez wakati akimfanyia faulo mshambuliaji wa Leeds jambo lililomfanya atolewe nje ya mchezo kwa kadi nyekundu. Picha na Mtandao

“Ulikuwa ni uamuzi wa kushtua kumtoa nje Licha (Lisandro Martinez). Hizi ni mechi mbili mfululizo tumekuwa na uamuzi wa aina hiyo dhidi yetu lakini hii ni mbaya zaidi kuwahi kuona.

“Nitakwenda kujadili hili lakini nadhani ni uamuzi mbaya,” amesema Carrick.

Carrick amedai pia mchezaji wake Leny Yoro alipigwa kiwiko katika mchezo huo lakini hakuna adhabu iliyotoka upande wa Leeds United.

“Unaweza kumpiga kiwiko Leny Yoro upande mmoja wa kichwa chake na pia ukarusha mkono wako katika uso wa Licha na akakosa balansi kwa sababu ya hilo. Kiasi fulani anagusa upande wa nyuma wa nywele zake.

“Ni mguso na anatolewa nje,” amesema Carrick.