Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mourinho apigiwa upatu kurejea Man United

Kocha wa Benfica, Jose Mourinho. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Carrick ameiongoza Man United kusogea hadi katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England msimu hadi sasa.

Kiungo wa zamani wa Manchester United, Nicky Butt amemtaja Jose Mourinho kama mtu sahihi wa kuwa Meneja wa kudumu wa timu hiyo.

Butt ametoa maoni hayo wakati Manchester United ikiwa katika mchakato wa kumsaka Meneja wa kudumu wa kuchukua nafasi ya Ruben Amorim ambaye alitimuliwa Desemba mwaka jana.

Tofauti na maoni ya wengi wakimtaja Kaimu Meneja wa timu hiyo kwa sasa Michael Carrick kuwa ndiye anastahili kuendelea kwa muda mrefu, Butt yeye fikra zake zipo kwa Mourinho.

Mourinho kwa sasa anaitumikia Benfica ya Ureno lakini aliwahi kuinoa Man United aliyoachana nayo mwaka 2018 baada ya timu hiyo kutopata ushindi katika mechi saba mfululizo.

Butt amesema kuwa sababu inayomshawishi ampendekeze Mourinho ni fikra chanya ya ushindi ambayo Mreno huyo anayo.

“Ningemrudisha (Mourinho). Ni mshindi na angeweza kuibeba klabu lakini walio katika madaraka hawawezi kuruhusu hilo kwa vile kwa sasa wanapendelea meneja anayejikita zaidi katika ufundishaji na sio usajili.

“Hakuna meneja aliyejijenga ambaye atakubali kuja Manchester United pasipo kuhakikishiwa bajeti, muda na utawala.

“Muundo wa sasa utatengeneza ugumu na inaonekana watapendelea awe Carrick,” amesema Butt.

Butt anaamini kazi iliyofanywa na Michael Carrick ndani ya muda mfupi itaupa wakati mgumu uongozi wa Man United katika mchakato wa kusaka meneja wa kudumu.

Carrick ameiongoza Man United kusogea hadi katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England msimu hadi sasa.