Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gallas azitabiria mazuri Arsenal, Man United

Muktasari:

  • Hata hivyo, Mfaransa huyo amebainisha habari mbaya kwa timu yake ya zamani ya Chelsea, kwa sababu anaamini nafasi ya mwisho ya tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka itashindaniwa na Spurs na Man United.

LONDON, ENGLAND. William Gallas anaamini kutakuwa na vuta nikuvute baina ya Tottenham na Manchester United katika kugomea nafasi kwenye Top Four katika Ligi Kuu England msimu huu.

Beki huyo wa zamani wa Chelsea na Arsenal anaamini mabingwa na Manchester City na The Gunners zitapata nafasi ya kujiwekea kibindoni tiketi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Gallas anaamini pia kocha mpya Arne Slot ataiongoza Liverpool kwenye kukamatia tiketi ya kucheza michuano hiyo mikubwa ya Ulaya mwakani kwa maana ya kumaliza Ligi Kuu England ndani ya Top Four.

Hata hivyo, Mfaransa huyo amebainisha habari mbaya kwa timu yake ya zamani ya Chelsea, kwa sababu anaamini nafasi ya mwisho ya tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka itashindaniwa na Spurs na Man United.

Alisema: "Nadhani kutakuwa na ushindani mkali sana kwenye Top Four ya msimu huu. Kitu kimoja ninachokifahamu kwa uhakika ni kwamba Arsenal na Manchester City zitakuwemo, hivyo hapo itaacha nafasi mbili ambazo zitakuwa na ushindi mkali.

"Nadhani Liverpool nao watakuwemo. Wana kocha mpya, lakini wachezaji wanafahamu mahitaji yanayohitajika kwenye ligi. Nawaweka kwenye Top Four msimu huu. Nadhani Tottenham wanaweza kuwamo. Manchester United nao wanaweza kuwamo, japo kuna vitu vichache vinatia shaka."

Newcastle United iliyocheza kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita, wakati Aston Villa iliyomaliza kwenye Top Four msimu uliopita, Gallas haoni kama zitafanya kitu na kuwamo kwenye timu nne za juu kwenye Ligi Kuu England msimu huu.

Gallas aliongeza: "Sidhani kama kutakuwa na sapraizi yoyote kama ilivyokuwa msimu uliopita kwa Aston Villa ilipomaliza kwenye nafasi ya nne. Villa itacheza kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, nadhani nao watakuwa na msimu sawa na ilivyokuwa kwa Newcastle msimu uliopita."