Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Geita Gold, Kagera Sugar zarejea Ligi Kuu

Muktasari:

  • Kagera Sugar inarudi Ligi kuu baada ya kucheza Championship kwa msimu mmoja na Geita Gold inafanya hivyo baada ya kuikosa Ligi Kuu kwa misimu miwili.

Dar/Mikoani. Geita Gold na Kagera Sugar leo Jumapili, Juni 7, 2026, zimerudi tena katika Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuibuka na ushindi kwenye mechi zao za Ligi ya Championship zilizochezwa leo katika viwanja na miji tofauti nchini.

Kagera Sugar inarudi Ligi kuu baada ya kucheza Championship kwa msimu mmoja na Geita Gold inafanya hivyo baada ya kuikosa Ligi Kuu kwa misimu miwili.

Geita Gold imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Songea United kwenye Uwanja wa Nyankumbu, Geita.

Ushindi huo wa leo umeifanya Geita Gold kufikisha pointi 71 ambazo zimeihakikishia kumaliza katika nafasi mbili za juu kwenye msimamo wa ligi ya Championship msimu huu.

Mabao yaliyopeleka furaha kwa Geita Gold katika mchezo wa jana yamefungwa na Maulid Shaban aliyepachika mawili na lingine la Richardson Ng'ondya. Songea United imepata bao lake la kufutia machozi kupitia kwa Seleman Seif.

Kitendo hicho cha Geita Gold kupanda Ligi Kuu kinamfanya Kocha wake Mkuu, Zuberi Katwila awe amepandisha daraja timu mbili ambapo ya kwanza ilikuwa ni Ihefu.

Nayo Kagera Sugar imepanda  Ligi Kuu baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kengold kwenye Uwanja wa Kaitaba, Kagera.

Baadhi ya wachezaji wa Kagera Suagar wakishangilia ushindi uliowarudisha tena dhidi ya Kengold. Picha na Kagera Sugar

Mabao ya Kagera Sugar yamefungwa na Obrey Chirwa, David Luhende na Kassim Feka. Ushindi huo umeifanya Kagera Sugar kufikisha pointi 68 na kuendelea kushika nafasi ya pili.

Kutokana na Polisi Tanzania kupoteza kwa bao 1-0 mbele ya Mbuni, Kagera Sugar imepanda Ligi Kuu kwa vile Polisi Tanzania haitoweza kufikisha pointi 68 ilizonazo sasa kwani ikishinda mechi mbili zilizobaki, itamaliza na pointi 66 kwa vile sasa ina pointi.