Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Himid Mao mlangoni Azam FC

Muktasari:

  • Taarifa za uhakika ilizopenyezewa Mwananchi  ni kwamba, Mao atasaini mkataba wa kuitumikia timu hiyo muda wowote kuanzia sasa baada ya makubaliano kati ya uongozi na mchezaji huyo kwenda vizuri huku uongozi ukiamini kuwa uzoefu wa mchezaji huyo utawasaidia.

Baada ya kushindwa kufikia malengo msimu huu uongozi wa Azam FC unaendelea kujipanga kwa ushindani msimu ujao ukisajili kimya kimya, tayari mabosi wa timu hiyo wanadaiwa kukamilisha usajili wa kiungo mkabaji Himid Mao.

Azam FC ambayo tayari imekamilisha usajili wa aliyekuwa kipa wao Aishi Manula, beki Lameck Lawi na Muhsin Malima wapo kwenye hatua za mwisho kumrudisha Mao ambaye amemaliza mkataba na waajiri wake wa zamani Tala'ea El Galish ya Misri.

Taarifa za uhakika ilizopenyezewa Mwananchi  ni kwamba, Mao atasaini mkataba wa kuitumikia timu hiyo muda wowote kuanzia sasa baada ya makubaliano kati ya uongozi na mchezaji huyo kwenda vizuri huku uongozi ukiamini kuwa uzoefu wa mchezaji huyo utawasaidia.

Mwananchi lilimtafuta kiungo huyo ili kuthibitisha taarifa hizo ambapo alisema sasa ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba na timu yake aliyoitumikia kwa msimu mmoja.

"Ni wakati wao kuzungumza chochote kunihusu kwa sababu ni mchezaji huru, sina mkataba na timu yoyote, kuhusu ofa ya Azam FC ni kweli kuna mazungumzo kati yetu lakini bado mambo hayajakamilika sitaweza kuzungumza lolote."

Azam inamrejesha Mao baada ya kiungo huyo kuihama 2018/19 alipojiunga na Petrojet ambayo aliitumikia kwa msimu mmoja na baadaye kujiunga na ENPPI.

Mao anayecheza nafasi ya kiungo mkabaji, amedumu misimu saba nje ya Tanzania akicheza soka la kulipwa sasa anatajwa kurejea tena nchini akiwa anatajwa kama mchezaji mzawa aliyedumu kwa muda mrefu zaidi nchini humu akiwa amezichezea timu saba.

Miongoni mwa wachezaji ambao hawakudumu katika Ligi Kuu ya Misri ni Emmanuel Okwi, Khalid Aucho na Gavin Kizito (Uganda), Luis Miquissone (Msumbiji), Walter Bwalya (Zambia) na Idrissa Mbombo (DR Congo).