Iran ilivyotumia mechi kuilaani Marekani
Baadhi ya wachezaji wa timu ya taifa ya Iran wakiwa wameshika mabegi ya shule wakati wimbo wao wa taifa ukipigwa kabla ya mechi dhidi ya Nigeria kama ishara ya kupinga shambulio lililotokea katika shule ya msingi siku ya kwanza ya vita vya Iran.
Berek, Uturuki. Timu ya taifa ya Iran juzi ilivaa vitambaa vyeusi mkononi na kushikilia mabegi ya shule wakati wimbo wao wa taifa ukipigwa kabla ya mechi dhidi ya Nigeria kama ishara ya kupinga shambulio lililotokea katika shule ya msingi siku ya kwanza ya vita vya Iran.
Shambulio katika shule ya Shajareh Tayyebeh mwezi uliopita liliua takribani watu 168, wakiwemo takriban watoto 110 kama ilivyoripotiwa na maofisa wa Iran.
Kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Nigeria, wachezaji wa Iran, akiwemo mshambuliaji wa zamani wa FC Porto na Inter Milan, Mehdi Taremi, walionekana wakiwa wameshika mabegi ya rangi ya waridi na zambarau yaliyofungwa utepe.
"Wachezaji wanashikilia mabegi ya shule karibu na nyoyo zao kwa kumbukumbu ya wasichana 165 waliouawa na Wamarekani katika shule ya Iran," alisema Ofisa Habari wa timu hiyo.
Katika mchezo huo wa kirafiki, Nigeria iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 yaliyofungwa na Moses Simon na Frank Onyeka huku lile la Iran likifungwa na Mehdi Taremi.
Maafisa wa Iran wameilaumu Marekani na Israel kwa shambulio hilo la shule, ambayo ilikuwa karibu na kambi ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), lakini hakuna kati ya nchi hizo iliyokubali kuwajibika.
Iran ni miongoni mwa nchi zilizofuzu kwa Kombe la Dunia mwaka huu, lakini ushiriki wao katika mashindano hayo, yatakayofanyika Marekani, Mexico na Canada kuanzia Juni 11 bado una mashaka.
Wamepangwa kuanza Kombe la Dunia dhidi ya New Zealand na Ubelgiji jijini Los Angeles kabla ya mchezo wao wa mwisho wa kundi dhidi ya Misri jijini Seattle.
Hata hivyo, Rais wa Marekani Donald Trump alisema mapema mwezi huu kwamba haitakuwa “sahihi” kwao kushiriki “kwa ajili ya maisha na usalama wao wenyewe.