Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kinachombeba Martinez kutwaa Ballon d’Or

Muktasari:

  • Martinez anayekipiga Inter Milan amekuwa katika kiwango bora akiibeba klabu yake ambayo ndiyo bingwa mtetezi wa Serie A, pia akiiwezesha Argentina kubeba taji la Copa Amerika.

Supastaa wa Argentina, Lautaro Martinez anatajwa kwenye orodha ya mastaa wanaoweza kushinda tuzo ya Ballon d’Or kwa msimu huu.

Martinez anayekipiga Inter Milan amekuwa katika kiwango bora akiibeba klabu yake ambayo ndiyo bingwa mtetezi wa Serie A, pia akiiwezesha Argentina kubeba taji la Copa Amerika.

Mbali na Martinez, wengine wanaotajwa kwenye tuzo hiyo ni winga wa Real Madrid na timu ya Taifa ya Brazil, Vinicius Junior na Jude Bellingham.


Takwimu akiwa na klabu

Akiwa na Klabu ya Inter Milan msimu uliopita wa 2023-24, Lautaro aliisaidia kutwaa ubingwa wa Italia Serie A, pamoja na Coppa Italia huku akitwaa tuzo ya Mfungaji Bora wa Ligi ya Italia akiwa na mabao 24.


Takwimu akiwa na timu ya Taifa

Akiwa na Argentina aliisaidia kutwaa Ubingwa wa Copa Amerika 2024, alipofunga bao pekee kwenye fainali dhidi ya Colombia ambapo alifunga mabao matano kwenye michezo sita aliyocheza na kumfanya awe mfungaji bora wa mashindano.

Kabla hajajiunga na Iter Milan, Martinez alikuwa akiichezea Racing Club ya Argentina ambako alicheza michezo 48, huku akifunga mabao 22, Julai 4, 2018 Martinez alijiunga na Inter Milan.

Mpaka sasa ameichezea Inter michezo 208, akifunga mabao 103, huku Argentina akicheza michezo 65 akipachika mabao 29.

Hii ni mara yake ya tatu kutajwa kwenye orodha ya wanaowania Ballon d’Or, ambapo alifanya hivyo mwaka 2021 na 2023, huku mwaka huu akionekana kuwa na nafasi nzuri ya kutwaa tuzo hiyo.