Kipa Chelsea akatwa mshahara wa wiki, aomba radhi

Muktasari:
- Kepa amelimwa faini ya Pauni 72 milioni jana Jumatatu ambazo ni mshahara wake wa wiki, huku uongozi wa klabu hiyo ukichukua hatua zaidi kwa kumjadili.
England. Kipa wa Chelsea, Kepa Arrizabalaga amepigwa faini kutokana na kitendo cha kugomea kutoka nje wakati kocha akifanya mabadiliko kwenye fainali ya Kombe la Carabao dhidi ya Manchester City mwishoni mwa wiki.
Kepa amelimwa faini ya Pauni 72 milioni jana Jumatatu ambazo ni mshahara wake wa wiki, huku uongozi wa klabu hiyo ukichukua hatua zaidi kwa kumjadili.
Kipa huyo aligoma kutoka nje ya uwanja ambapo nafasi yake ilitakiwa kuchukuliwa na Willy Caballero.
Hata hivyo kipa huyo ameomba radhi kwa Kocha Maurizop Sarri pamoja na wachezaji wnzake baada ya kugoma kufanyiwa mabadiliko kwenye mechi yao ya fainali ya Carabao Cup mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mchezaji huyo amejikuta akipigwa faini kwa kukatwa mshahara wa wiki kutokana na kitendo cha kukaidi uamuzi wa kocha kwenye dimba la Wembley.
Hata hivyo, kipa huyo ameomba radhi akisema amejifikiria kwa kina juu ya kitendo alichokifanya cha kugomea uamuzi wa kocha akisema kulikuwa hakuna maelewano kwa jambo lililotokea na amefanya kosa kubwa.
Amesema, ameamua kuomba radhi kwa dhati kwa kocha wake, kipa mwenzake pamoja na wachezaji wenzake pamoja na uongozi wa klabu.
Pia amesema anawaomba radhi mashabiki wa klabu hiyo na kueleza kuwa amejifunza kupitia tukio hilo na yupo tayari kutumikia adhabu yoyote itakayotolewa au hatua za kinidhamu ambazo klabu yake itaamua kuchukua.
Pia vigogo a Chelsea wameonya tukio hilo lisije kujitokeza tena kama ilivyowahi kuwa kwa Antonio Conte na Diego Costa mwaka 2017.