Ligi Kuu England imemalizika hivi

Muktasari:
- City imetwaa ubingwa huo na kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kwenye ligi hiyo kutwaa ubingwa huo mara nne mfululizo.
London, England, Ligi Kuu England ilimalizika juzi kwa Manchester City kufanikiwa kutwaa ubingwa baada ya kuichapa West Ham mabao 3-1 kwenye mchezo wa mwisho.
City imetwaa ubingwa huo na kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kwenye ligi hiyo kutwaa ubingwa huo mara nne mfululizo.
Baada ya ligi hiyo kumalizika, zimewekwa rekodi kadhaa kali kwenye ligi hiyo na kuna timu ambazo zimefanya mambo makubwa na ya kushangaza, lakini pia kuna rekodi za jumla za ligi hiyo.
Zilizofuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya
Manchester City, Liverpool, Arsenal na Aston Villa.
Iliyofuzu Europa
Tottenham Hotspur
Zilizoshuka
Luton Town
Burnley
Sheffield United
Timu zilizochukua ubingwa mfululizo:
4 - Manchester City (2020/21 - 2023/24)
3 - Manchester United (2006/07 - 2008/09)
3 - Manchester United (1998/99 - 2000/01)
2 - Manchester City (2017/18 - 2018/19)
2 - Chelsea (2004/05 - 2005/06)
2 - Manchester United (1995/96 - 1996/97)
2 - Manchester United (1992/93 - 1993/94)
Mabao kipindi cha kwanza
19: Mechi za mwisho za msimu zilishuhudia mabao 19 yakifungwa kwenye kipindi cha kwanza cha mchezo yakiwa ni mengi kuliko vipindi vingine vyote kuanzia Oktoba 3 mwaka 1992, yalipofungwa mabao 21.
Mabao 1,223
Mabao 1,223 yamefungwa kwenye msimu huu wa Ligi Kuu England yakiwa ni mengi zaidi kuwahi kutokea tangu 1,222, yalipofungwa msimu wa 1992-93, wakati timu zikiwa 22.
Guardiola sita
6- Pep Guardiola emetwaa makombe sita kwenye Ligi Kuu England, akiwa ni kocha wa nne kufikisha zaidi ya makombe matano ya ligi hiyo baada ya Sir Alex Ferguson (13), George Ramsay (6) na Bob Paisley (6).
Klopp mmoja tu
Kocha wa Liverpool Jürgen Klopp ameweka rekodi ya kuwa meneja wa kwanza kwenye timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England, Ligi ya Mabingwa Ulaya, Kombe la FA na Kombe la Ligi.
Wamejifunga 49
Msimu wa Ligi Kuu England umemaliza huku mabao 49 yakitokea kwa wachezaji kujifunga yakilingana na yale ya msimu wa 2013-14.
Ole Watikns atisha

Mshambuliaji wa Aston Villa, Ollie Watkins wa Aston Villa amemaliza msimu akiwa kinara wa kutoa pasi za mabao (asisti), baada ya kupiga 13 anafuatiwa na Cole Palmer wa Chelsea mwenye 11.
Rodri mwamba kwelikweli
Staa wa Manchester City, Rodri ameweka rekodi ya kupiga pasi 3,633, akiwa ndiye kinara, akifuatiwa na Lewis Dunk wa Brighton aliyepiga 3,212.
Sheffield United hoi
Klabu ya Sheffield United imemaliza msimu ikiwa imepoteza michezo 28 kati ya 38 msimu huu, tayari timu hiyo imeshashuka daraja.
Joao Palhinha, nidhamu mbovu
Beki huyo wa Fulham ameweka rekodi ya kupewa kadi nyingi za njano baada ya kukusanya 13, sawa na Marcos Senese wa Bournemouth, mchezaji wa tatu ni Douglas Luiz wa Aston Villa. Yves Bissouma wa Tottenham Hotspur yeye ameongoza kwa kadi nyekundu baada ya kulambwa mbili, sawa na Reece James wa Chelsea.
Alfie Doughty afanya yake Luton
Kiungo wa Luton, Alfie amemaliza msimu akiwa kinara wa kupiga krosi baada ya kupiga 340 kwenye michezo 36 aliyocheza, anafuatiwa na Pascal Groß wa Brighton & Hove Albion ambaye amepiga 238.
Erling Haaland na huku yupo

Baada ya mshambuliaji huyo wa Man City kumaliza msimu akiwa kinara wa ufungaji na mabao 27, pia ameweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyepiga mashuti mengi yaliyolenga lango kwenye ligi hiyo baada ya kupiga 59 akifuatiwa na Mohammed Salah wa Liverpool aliyepiga 56.
Onana katisha United

André Onana wa Manchester United ameweka rekodi ya kucheza michezo yote 38 msimu huu akiwa sawa na wachezaji wengine 14 kwenye ligi hiyo.