Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majambazi wavamia kijiji, wapora fedha

Muktasari:

  • Watu wanaosadikiwa ni majambazi wamevamia nyumbani kwa mfanyabiashara Mustapha Gea (25) mkazi wa Kijiji cha Nduruka, Wilaya ya Liwale mkoani Lindi na kupora bidhaa zikiwemo simu za mkononi, vocha na fedha taslimu.

Lindi. Watu wanaosadikiwa ni majambazi wamevamia nyumbani kwa mfanyabiashara Mustapha Gea (25) mkazi wa Kijiji cha Nduruka, Wilaya ya Liwale mkoani Lindi na kupora bidhaa zikiwemo simu za mkononi, vocha na fedha taslimu.

Taarifa kutoka kwa baadhi ya mashuhuda na wakazi wa kijiji hicho, pamoja na kuthibitishwa na mamlaka husika ya Serikali mkoani Lindi, zinaeleza uhalifu huyo umefanyika usiku wa kumakia Agosti 8, 2021.

Karimu Issa ameeleza siku hiyo, kundi la watu wasiopungua saba wakiwa na silaha zikiwemo za moto, walifika nyumbani kwa mfanyabiashara Gea na kuvunja mlango kwa kutumia jiwe maarufu kwa jina maarufu la Fatuma na kuingia ndani.

Kamanda wa Polisi Mkoani Lindi, ACP Mtatiro Kitinkwi amethibitisha kutokea kwa uhalifu huo katika Kijiji hicho na kueleza majambazi hayo yamepora simu mbili aina ya Intel na Sumsung, vocha za Halotel, Tigo, Zantel, kadi za benki za CRDB, NMB, vitambulisho vya kupigia kura na fedha taslimu zaidi ya Sh5.24 milioni.