Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United, Spurs vita ya Ubingwa Europa

Muktasari:

  • Mara ya mwisho United ilichukua taji hilo mwaka 2017 wakati Tottenham ikifanya hivyo mwaka 1984.

Kesho Jumatano, macho ya mashabiki wa soka duniani yataelekezwa Bilbao, Hispania, pale ambapo Manchester United na Tottenham watawania taji la Europa League katika mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa San Memes.

Tayari timu zote zimeshaelekea nchini Hispania, huku United wakiwa wametupia suti maalumu zilizotengenezwa na mwanamitindo Paul Smith zenye thamani ya Pauni 1,000 kwa kila suti sawa na Sh3,578,290, kwa pesa ya Kitanzania, huku Spurs wakishuka Hispania wakiwa wamepiga track Suit maalumu ambazo zimeandaliwa na kampuni ya Nike ambayo imekuwa ikifanya kazi na timu hiyo.

"Man United hawawezi kutusumbua, pamoja na nafasi tuliyopo kwenye ligi tumefanya vizuri kwenye michezo tuliyokutana, nafikiri ni fainali ya upande wetu," aliandika shabiki wa Spurs.

Man United inataka kwenda kuwapa raha mashabiki wao baada ya kufanya vibaya kwenye Ligi Kuu England kwa kubeba taji la Ulaya katika fainali hiyo ya Bilbao, usiku wa leo Jumatano.

Msimu huu umekuwa wa changamoto kwa timu zote mbili, hasa kwenye ligi zao za nyumbani ambapo United inashika nafasi ya 16 wakati Spurs ikifuatia katika nafasi ya 17 lakini fainali hii ni nafasi yao ya kufutia machozi, na kuwapa furaha mashabiki wao baada ya msimu mbaya.

Hata hivyo, bado kuna hofu kuwa kocha yoyote anayeweza kupoteza mchezo huu kibarua chake kitakuwa shakani.

Manchester United msimu huu umekuwa wa taabu kwao kwani wamepoteza mechi 18 katika ligi kuu, idadi kubwa ambayo hawajawahi kuifikia tangu msimu wa 1973-74.

Kwa upande wa Tottenham wamepoteza mechi 25 katika mashindano yote msimu huu, rekodi mbaya zaidi katika historia yao. Katika Ligi wamepata ushindi mmoja tu kati ya mechi 11 za mwisho.

Tottenham wanakumbwa na changamoto kubwa za majeraha, huku wachezaji muhimu kama Dejan Kulusevski na James Maddison wakikosa fainali hii kutokana na majeraha. Hata hivyo, mshambuliaji wao Son Heung-min anatarajiwa kucheza katika fainali hiyo baada ya kuwa fiti.

Kocha, Ruben Amorim amewaonya wachezaji wake kuwa hakuna atakaye wakumbuka iwapo wakipoteza fainali hiyo. Amorim anaamini kwamba ni mchezo ambao United inapaswa kushinda.

"Jambo nililojifunza nikiwa mchezaji ni kwamba lazima ushinde," amesema Amorim."Hakuna atakayesema 'nilifika fainali', hasa ukiwa katika klabu ya aina hii. Hivyo basi, tunahitaji kushinda fainali.

"Ni jambo muhimu sana kwetu, tunataka kuwapa mashabiki wetu zawadi hiyo. Nimejaa hamasa, lakini wakati huohuo, najua wajibu wangu kama kocha wa Manchester United.

"Daima ninabeba hisia za kukatishwa tamaa kutokana na msimu huu, hivyo ninataka kuisaidia timu kushinda fainali hii. Tunapaswa kutoa kitu kwa klabu yetu na kwa mashabiki," amesema Amorim kocha wa United.

Tottenham wataingia kwenye mchezo huo na kumbukumbu nzuri ya kuichapa United katika michezo yote miwili ya Ligi Kuu msimu huu ambapo ilipata ushindi wa mabao 3-0 kwenye mechi ya kwanza iliyofanyika Old Trafford huku ikishinda bao 1-0 katika mchezo wa pili walipokuwa nyumbani.

Manchester United wamefika katika fainali ya Europa League mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2021, ambapo walinyanganywa taji hilo na Villarreal baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penalti 11-10 katika fainali iliyopigwa kwenye Uwanja wa Gdańsk, Poland.

Mara ya mwisho United ilichukua taji hilo mwaka 2017, baada ya kuifunga Ajax mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Strawberry, Sweden.

Kwa upande wa Tottenham wamechukua taji hili mara mbili wakifanya hivyo mwaka 1972 walipoifunga Wolverhampton jumla ya mabao 2-1 na mwaka 1984 wakiifunga Anderlecht kwa mikwaju ya penati 4-3.

Tottenham ilitinga katika hatua ya fainali baada ya kuiondoa Bodo/Glimt kwa jumla ya mabao 5-1, ikishinda 2-0 ugenini na kupata ushindi wa mabao 3-1 nyumbani.

Manchester United ilitinga katika fainali baada ya kuwaondoa Atletic Bilbao kwa jumla ya mabaa 7-1 ambapo United ilishinda mabao 3-0 ugenini kabla ya kuandika ushindi mwingine wa mabao 4-1 kwenye uwanja wa nyumbani