Mapenzi kumstaafisha Fraser-Pryce

Muktasari:

Fraser-Pryce anatarajiwa kuwa miongoni mwa nyota watakaoipeperusha bendera ya Jamaica katika michezo ya Olimpiki mwaka huu katika mbio za mita 100. Mita 200 na mita 400 kupokezana vijiti

Dar es Salaam. Mkali wa mbio fupi upande wa wanawake, Shelly-Ann Fraser-Pryce ametangaza kuwa atastaafu rasmi riadha baada ya michezo ya Olimpiki mwaka huu huko Ufaransa ili apate muda wa kufurahia maisha na mapenzi na mume wake pamoja na mtoto wake.

Fraser-Pryce anatarajiwa kuwa miongoni mwa nyota watakaoipeperusha bendera ya Jamaica katika michezo ya Olimpiki mwaka huu katika mbio za mita 100. Mita 200 na mita 400 kupokezana vijiti.

Mwanariadha huyo amesema katika kipindi ambacho amekuwa akishiriki mbio, ukaribu na familia yake umetetereka hivyo anataka kuwapa fura ya kuwa pamoja mara baada ya kumalizika kwa Olimpiki.

"Mtoto wangu wa kiume ananihitaji. Mume wangu na mimi tumekuwa pamoja kabla hata sijashinda mwaka 2008. Amejitoa sadaka kwa vingi kwa ajili yangu. Sisi ni washirika, ni timu.

"Ni kwa sababu ya sapoti hiyo ninaweza kufanya vitu ambavyo nimekuwa navifanya kwa miaka yote hii.Na sasa nawaachia wao nafasi ya kufanya ktu kingine," amesema mwanariadha huyo.

Fraser-Pryce ameshinda medali 2 za dhahabu katika mbio za mita 100, kupokezana vijiti na zile za mita 200 katika mashindano tofauti aliyowahi kushiriki.

Idadi kubwa ya medali za dhahabu amezipata katika mashindano ya dunia na amefanya hivyo mara 10, akishinda dhahabu tatu kwenye Olimpiki na medali tano katika Ligi ya Diamond.