Matano, Ouma wataka VAR Ligi Kuu

Muktasari:
- Kuna vitu vinatokea uwanjani hasaa kwenye soka ,ambavyo vinabadili matokeo ya mchezo na kuathiri matokeo kwa jumla,
Kuna vitu vinatokea uwanjani hasaa kwenye soka ,ambavyo vinabadili matokeo ya mchezo na kuathiri matokeo kwa jumla, kwa mfano; Kocha wa wana mvinyo wa Tusker Robert Matano alionekana mwenye hasira baada ya mechi yao dhidi ya Gor Mahia, huku akinyoosha kidole cha lawama kwa mwamuzi wa katikati Antony Ongwayo kwa kufanya maamuzi ambayo yaliegemea upande wa Gor Mahia siku ya Jumamosi .
Kwenye kanda hiyo ya video ,Jackson Macharia alionekana kufungia Tusker bao dakika za lala salama kipindi cha pili lakini bao hilo likakataliwa hii ni baada ya mwamuzi wa tatu wa mechi hiyo kuinua kijibendera ishara kuwa mchezaji mmoja kutoka timu ya Tusker alikuwa tayari ameotea .
Matano aidha alitumia maneno makali kukashifu maamuzu hayo ;
‘Refa huyu hafai hata kufanya mafunzo zaidi ya urefa ,yafaa apigwe marufuku kabisa kujihusisha na michezo yoyote ya Ligi Kuu .Awaachie marefa wengine kazi ambao wanauwezo wa kufanya maamuzi ya kweli bila kuangalia upande mmoja .Nimekuwa kwa soka kwa miaka mingi lakini sijayaona mambo kama haya yakifanyika kwa soka yetu .’Alisema Matano .
Alipoulizwa ikiwa atakata rufaa kuhusiana na uamuzi huo ,alikataa kivali .
‘Siwezi kata rufaa kwa mambo kama haya ,wenyewe wafanye wanavyo taka lakini mchezo wa kisasa hauchezwi hivyo maamuzi kama haya yanauwa soka yetu . Mwamuzi wa mechi yoyote anapofanya maamuzi yake ni lazima ajiamini kwa kile anachofanya kama ni bao awape waliofunga bao lao, hata rais wa FIFA hawezi zuia refarii kufanya maamuzi yake uwanjani .’ Aliongezea Matano
Kwa upande wa kocha wa timu ya Sofapaka David Ouma pia, alionekana kutoridhishwa na maamuzi ya refa wakati wa mechi yao dhidi ya Kakamega Homeboyz katika uga wa Kasarani Annex siku ya Jumapili.
Mechi hiyo ambayo iliisha sare ya 1-1 ,kocha Ouma anasema kuwa marefarii waadhibu wachezaji kulingana na makosa ambayo wanafanya bila kuegemea timu ambazo zinaongoza Ligi .
‘Sheria za soka zifuatwe ,nimekubali wachezaji wangu kukabwa wakati wanapocheza lakini mchezaji anapochezewa vibaya kutoka nyuma na kuanguka yafaa maamuzi yafanyike papo hapo bila kuegemea upande mmoja .Wachezaji wetu lazima wafunzwe wakiwa Kenya iliwatakapo enda nje kucheza wawe makini kuepukana na makosa ambayo yatawaweka taabani na waamuzi wa mechi .’Alisema Ouma
Aidha amewaomba waamuzi wa mechi za Ligi Kuu kuwa makini wanapofanya maamuzi yao uwanjani wakati wa mechi .
Tangia ujio wa VAR mwaka 2019 Ligi Kuu ya uingereza ,imekuwa ni njia moja ya kuwasaidia marefa kufanya maamuzi ambayo hayaegemei upande mmoja na pia imewasaidia kutoa maamuzi halali wakati wa mechi .Tumeona pia zikitumika wakati wa mechi za kombe la dunia, pia Afrika wakati wa muchuano ya AFCON.