Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbrazili kaanza mkwara Simba, ataka mastaa wote kambini

Muktasari:

  • JANA  usiku Simba ilijitupa kwenye Uwanja wa Amaan Zanzibar kucheza mchezo wa mwisho wa Kombe la Mapinduzi kwa msimu huu dhidi ya KVZ, huku kocha mkuu mpya, Mbrazil Roberto Oliveira ‘Robertinho’ tayari ameiona timu na kupiga mkwara akiwataka wachezaji wote kambini fasta.

JANA  usiku Simba ilijitupa kwenye Uwanja wa Amaan Zanzibar kucheza mchezo wa mwisho wa Kombe la Mapinduzi kwa msimu huu dhidi ya KVZ, huku kocha mkuu mpya, Mbrazil Roberto Oliveira ‘Robertinho’ tayari ameiona timu na kupiga mkwara akiwataka wachezaji wote kambini fasta.

Robertinho alitambulishwa na Simba juzi akitokea Vipers ya Uganda na kupanda boti moja kwa moja kwenda Zanzibar ambako alikuwa jukwaani wakati chama lake hilo jipya likichapwa bao 1-0 na Mlandege na kuvuliwa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi ililolibeba msimu uliopita na baada ya mechi ile kumalizika aliuambia uongozi anataka kuwaona wachezaji wote hata ambao hawakuwepo uwanjani ili akae nao.

Uongozi wa Simba ulichukua kwa ukubwa maagizo hayo ya kocha na baada ya mechi ya leo, Simba kesho asubuhi itarejea Dar es Salaam na moja kwa moja itaingia kambini chini ya Robertinho atakayeanza rasmi kukisoma kikosi na kuelekeza mbinu zake.

Taarifa za ndani ya Simba zinaeleza kocha huyo ametaka siku 10 tu za kukaa na wachezaji, kutambulisha mbinu na mifumo yake na pia ameutaka uongozi kumtafutia mechi zisizopungua tatu za kirafiki ili kukamilisha mipango yake tayari kwa mapambano atakayoanza Januari 17 katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kocha huyo ambaye ni muumini wa soka la kushambulia kuanzia nyuma kwa pasi nyingi pia ameuambia uongozi anataka kuongezewa nguvu katika benchi la ufundi kwa kuleta kocha msaidizi mwingine ambaye ni chaguo lake atakayesaidiana na Juma Mgunda.


Chama, Phiri mmh

Wakati Robertinho akiwataka wachezaji wote kambini, viongozi wa Simba wameanza kuumiza vichwa namna ya kuwarudisha ghafla mastaa wake ambao walikuwa wamewapa mapumziko mafupi na walio majeruhi wakiwemo Wazambia wawili Clatous Chama na Moses Phiri ambao wapo nchini kwao.

Chama ambaye ni kinara wa asisti kikosini hapo akiwa nazo 11, alipewa mapumziko ya siku zisizopungua saba.