Mbunifu jezi mpya Yanga afunguka

Mbunifu jezi mpya Yanga afunguka

Muktasari:

  • MBUNIFU wa jezi mpya za Yanga, Sheria Ngoi amesema jezi aliyoibuni maalumu kwa msimu wa mwaka 2021/22 haitakuwa na mpinzani sio kwa Tanzania tu hadi mataifa makubwa.

MBUNIFU wa jezi mpya za Yanga, Sheria Ngoi amesema jezi aliyoibuni maalumu kwa msimu wa mwaka 2021/22 haitakuwa na mpinzani sio kwa Tanzania tu hadi mataifa makubwa.

Akitolea ufafanuzi jezi ya nyumbani amesema wao ni wananchi hivyo kwenye jezi wameonyesha namna wananchi wanavyotakiwa kujiona.

Mbunifu jezi mpya Yanga afunguka

Akizungumzia jezi ya ugenini ambayo ina rangi ya njano ina watu waliokaa kwenye makundi hivyo inaonekana kwa tofauti ya rangi.Nyeusi ni maalumu kwaajili ya kusafiria itatumika kwaajili ya benchi la ufundi sambamba na jezi ya kimataifa yenye lebo ya mistari 27 ambayo imesimama kwaajili ya kuwakilisha makombe walitowahi kutwaa Yanga.

Pia ametolea ufafanuzi jezi ya wachezaji maalumu kwaajili ya safari ambayo imeonyesha barabara katikati ikiwakilisha safari.

Ametolea ufafanuzi jezi za safari kwa upande wa viongozi ambazo zina kola tofauti na ya wachezaji.