Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Paredi la ubingwa Yanga laibua mambo

Dar es Salaam. Wakati Yanga ikisherehekea ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa kufanya paredi leo Jumamosi ya Julai 4, 2026, mashabiki kadhaa wa timu hiyo wameonekana Kutoridhishwa na utaratibu uliotumika wa maandalizi hayo.

Katika maeneo ya Karume jijini Dar es Salaam, ambapo paredi hilo linaanzia, mashabiki hao wameonyesha hali ya wasiwazi na kutoridhishwa na maandalizi hayo yanayoendelea hadi sasa.

Mashabiki hao wamekuwa wakikosoa utaratibu uliotumika kuweka eneo la Karume ambalo wanaamini ni dogo na halina hadhi kwa kuanzisha paredi hilo kama ilivyokuwa utaratibu wa misimu yote inayofanya kikosi hicho kilipotwaa ubingwa.

Kwa misimu ya hivi karibuni, shughuli hizo zimekuwa zikianzia Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, japo safari hii mambo yamekuwa ni tofauti na inaanzia Karume, ikipita Msimbazi iliko makao makuu ya Simba na kuhitimisha mitaa ya Twiga na Jangwani yalipo makao makuu ya kikosi hicho.

Mbali na hilo ila mashabiki hao pia wamekosoa utaratibu wa muda uliotangazwa na kinachoendelea kwa sasa, ambao wanaona ni kutotendewa haki ya kuendana na muda uliopangwa.

Minong'ono hiyo inajiri baada ya uongozi wa Yanga kutangaza paredi hilo litaanza saa 4:00 asubuhi, ingawa hadi sasa saa 11:40, bado halijaanza.