Pascal Msindo ajifunga miaka miwili Azam FC
Muktasari:
- Mkataba wa awali wa Msindo na Azam FC ulikuwa ufikie tamati mwishoni mwa msimu ujao na sasa beki huyo wa kushoto mwenye umri wa miaka 20 ameamua kuendelea kuipan huduma zaidi timu hiyo
Beki Pascal Msindo leo amesaini mkataba mpya wa miaka miwili utakaomuweka klabuni hapo hadi 2027.
Mkataba wa awali wa Msindo na Azam FC ulikuwa ufikie tamati mwishoni mwa msimu ujao na sasa beki huyo wa kushoto mwenye umri wa miaka 20 ameamua kuendelea kuipan huduma zaidi timu hiyo.
Taarifa ya kusainiwa kwa mkataba mpya baina ya pande hizo mbili, imetolewa leo na Azam FC kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.
"#ContractExtension Beki wetu mahiri wa kushoto, @pascalmsindo, ataendelea kusalia kwenye viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2027, baada ya kuongeza mkataba mpya wa miaka miwili," ilifafanua taarifa ya Azam FC.
Msindo alijiunga na kikosi cha wakubwa cha Azam FC mwaka 2022 baada ya kuonyesha kiwango bora katika timu ya vijana ya klabu hiyo ambayo ilimnasa kutokea kituo cha kulea na kuibua vipaji vya soka cha Moro Kids cha Morogoro.
Mbali na Aam FC, Msindo pia anatumikia kikosi cha timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 na mara kadhaa amewahi kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya wakubwa 'Taifa Stars'.